When it suits them....
Sina uhakika na wenzetu wa Nyumbani ila wengi wetu wa Ughaibuni (wanawake) tunalaliwa na Wanaume tunaoishi nao aka Wenza/Waume.
Maisha ya Ughaibuni ni Magumu sana japokuwa upatikanaji wa vitu basic ni rahisi.....kwamba huwezi kuvaa nguo/viatu vilevile au kutumia Friji/Jiko/Kochi lilelile kwa miaka mitatu.
Lazima kutakuwa na hitaji la kununua vipya(ni kwasababu ubora wake ni wa chini) lengo la Makampuni mengi nikuwawezesha Wananchi "wa kawaida" kumudu vitu ambavyo vinafanya maisha yao kuwa rahisi(kurahisisha maisha).
Au tuseme ni "kiwango cha ubora wa maisha" kwa kila mwananchi kilichowekwa na Serikali.......sasa ukiamua kuibuka na Sumsang Fridge sababu unamudu hakika utakuwa nayo kwa miaka 10 zaidi.
Turudi kwenye Kichwa cha Habari; Ughaibuni sote tunafanya kazi (mimi bado ni Temp Mama wa kunyumba)na tuna-share majukumu Kiuchumi lakini linapokuja suala la majukumu ya kuangalia/kulea watoto tunaambia ni "jukumu la mama".
Kwamba mimi baba nitacheza nao na "kuwakalipia" i mean kuwafunza lakini suala la kuhakikisha wamekula kwa wakati, wameoga na kuwa-assist back to bed wakiota majinamizi ni kazi ya Mama.
Sasaaaa kama maisha ya leo ni kusaidiana iweje Mkimama akusaidie majukumu yako (Kuleta pesa nyumbani na kulipa bills) wakati wewe Mkibaba una chill tu linapokuka suala mahitaji ya watoto?
Maisha ya sasa ni tofauti na yale ya bibi zetu....maana Wazazi wangu walisaidiana na baba yangu alikuwa hands on....alituogesha Uwani pale juu ya Karo sio bafuni na alitupikia kila weekends....yeah na tulikuwa na Wasaidizi x2.
Natambua baadhi yetu (well mie) tunapenda kufanya kila kitu na Mume akijaribu kusaidia unahisi kama vile hafanyi kwa usahihi......si wajua kala kautaratibu ulikojiwekea na watoto wamekazoea?
Lakini nikiwa nimelala na mtoto kaamka baada ya kuota anakimbizwa na Mamba au anakiu tafadhali deal with it....usiniamshe, unless ni emergency!
Kuna baadhi ya wanawake Ughaibuni ni Single Mothers with a hubby.....aii si bora ukanunue sex when you need it...kuliko kuwa na limwanaume linalotaka "kusaidiana" kwenye kulipa bills tu.
Babai.
Comments