Skip to main content

Posts

Showing posts with the label madoa

Namna ya Kuondoa Mdoa(Tetekuwanga) Usoni.....

....haraka! Najua kuwa unajua napenda ku-share kile ambacho nimejifunza na kwa sehemu kubwa ni kutokana na Uzoefu. Kwabahati mbaya niliugua Tetekuwanga(ililetwa na Schooler boy wangu). Kwasababu yeye ni Mtoto haikuwa mbaya kama mie Mtu mzima. Hii ndio nikawa naitumia Asubuhi na Usiku kama mbadala ya hiyo hapo chini Lancome Genifique ndio Serum yangu Kitambo. Mbaya zaidi Mapele yakajitokeza kwa Wingi Usoni( sijui kwanini hayakwenda Mapajani au Tumboni au Miguuni)....unapopata tatizo la Ngozi mahali ambapo sio rahisi kuficha inakupotezea Amani kabisa yaani. Hakuna Dawa ya kuondoa Mdoa hayo kwa haraka(inachukua Miezi 2 mpaka Miaka kadhaa inategemea madoa yapo deep kiasi gani Ngozini). Dactor niliandikiwa dawa ya kuondoa Madoa(mie naita Mkorogo) lakini baada ya siku chache nikahisi inaharibu ngozi yangu kwa namna nyingine, kwamba inaondoa Mdoa Meusi Usoni lakini "pores" zinapanuka/zinakuwa kubwa(sijawahi kuziona pores zangu) nikaamua kuachana nayo.