Skip to main content

Posts

Showing posts with the label ndivyo

Kujiamini kwa Mtoto kunaanza lini?

....Watoto wa "Ulaya" wanajiamini sana, je kuna namna ya kulea mtoto ili akikua ajiamini kama wa Ulaya? Mkaka mmoja aliniuliza. Nadhani wengi wetu tumeaminishwa Mengi ya Ughaibuni ni Mazuri/Mema....lakini katika hali halisi sivyo. Kuna soko zuri sana la Vitabu/Vipindi vya TV vinavyofunza Wazazi namna ya kulea watoto wenye Kujiamini. Ni tatizo la Wazazi husika ambao walilelewa "Kimaendeleo" na hivyo kuhofia kuwa watoto wao watakuwa kama wao. Hofu hiyo inawafanya wazazi kuwa-overprotect watoto. Nahisi tu sina uhakika. Kujiamini kunategemea zaidi na Malezi(nakubali) lakini sehemu kuwa ya Mtu/Mtoto kujiamini inatokana na yeye mwenyewe alivyoumbwa. Niliwahi kugusia Bloguni hapa kuwa kuna baadhi tumezaliwa hivyo(tunajiamini) lakini pia wapo ambao hawajiamini mpaka wafunzwe/himizwa/pewa Moyo/saidiwa kujiamini. Naamini Watoto wa Afrika(well Tanzania wa kizazi kileeee) tunajiamini kwasababu tulitumia muda mwingi kujifunza kimwili na sio kihisia kama watoto