....Sosho Midia si imewabadilisha? Hakika bado wapo hivyo ila namna wafanyavyo ni tofauti na walivyokuwa wakifanya kabla ya Sosho Midia(nionavyo mimi). Unakumbuka ulipokuwa mdogo(au ni mimi tu), Baba yako akisikia jambo kutoka kwa Mwanaume mwenzie halizungumzii ila anakwenda kwa huyo Mtu na kuzichapa/kumkung'uka Magumi? well Baba yangu alikuwa mtu Mwema na Mtu wa watu lakini alikuwa Ngumi Mkononi, anakutandika halafu yanaisha. sasa hii ndio "Wanaume hawakai na Kingongo" niijuayo mie. Niliendelea kuona hiyo kwa Kaka zangu na rafiki zao pia na hivyo kuweka Sementi kwenye hilo. Siku hizi Waanaume, wanaanika mambo ya wenzao nje (mitandaoni)ikiwa wamekorofishana, kwamba mmoja akiudhiwa/kasirishwa na mwenzie basi Jamaa wa Shosho Midia wote watajua. Kwa sisi Wanawake ambao hufikiria baada ya action(sio kabla) na kisha kuomba msamaha baada ya kuharibu ni Kawaida(ilizoeleka hivyo), lakini sio kwa Wanaume. Sio kwamba nasikitika kuwa Wanaume wamebadilika na wala s