Skip to main content

Posts

Showing posts with the label opinion

Ujidhaniavyo sivyo....

Heiyaaa. Mara zote huwa tunaamini tupo vile ambavyo hatupo. Nitakupa mfano:-  Unapoenda kununua Foundation(matope ya kupaka Usoni kabla ya mengineyo) unachagua rangi ambayo sio yako na huwa waaaay lighter. Sio kwamba unakusudia bali hutaki kukubali ile yako ambayo pengine inaonekana ni nyeusi sana kwenye Chupa kuliko unavyoamini(kithihitisho ni Picha zako). Enzi nilikuwa na "Wifi" wa Kiarabu na kwenye familia yao kulikuwa na waliozaliwa nje ya "uarabu" kwamba mzazi mmoja alikuwa Muarabu mwingine Mweusi halafu mtoto (binti) katokea mweusiiii mwenye nywele za kiarabu. Basi tukijikusanya tumapiga stori huyo binti alikuwa anapenda kuwasema wadada wengine kuwa ni Weusi mno kiasi kwamba hawavutii. Kwasababu mzazi wake mmoja ni Muarabu na anaishi kwenye Familia Kiarabu aliamini kuwa na yeye ni Muarabu. Hiyo pia huwatokea watoto waliochanganya na Wazungu na kuishi Uzunguni zaidi kuliko Weusini...huwa wanajidhania kuwa ni Wazungu(rangi wise). Kingine ni uwingi wa nywel