Heiyaaa.
Mara zote huwa tunaamini tupo vile ambavyo hatupo. Nitakupa mfano:- Unapoenda kununua Foundation(matope ya kupaka Usoni kabla ya mengineyo) unachagua rangi ambayo sio yako na huwa waaaay lighter.
Sio kwamba unakusudia bali hutaki kukubali ile yako ambayo pengine inaonekana ni nyeusi sana kwenye Chupa kuliko unavyoamini(kithihitisho ni Picha zako).
Enzi nilikuwa na "Wifi" wa Kiarabu na kwenye familia yao kulikuwa na waliozaliwa nje ya "uarabu" kwamba mzazi mmoja alikuwa Muarabu mwingine Mweusi halafu mtoto (binti) katokea mweusiiii mwenye nywele za kiarabu.
Basi tukijikusanya tumapiga stori huyo binti alikuwa anapenda kuwasema wadada wengine kuwa ni Weusi mno kiasi kwamba hawavutii. Kwasababu mzazi wake mmoja ni Muarabu na anaishi kwenye Familia Kiarabu aliamini kuwa na yeye ni Muarabu.
Hiyo pia huwatokea watoto waliochanganya na Wazungu na kuishi Uzunguni zaidi kuliko Weusini...huwa wanajidhania kuwa ni Wazungu(rangi wise).
Kingine ni uwingi wa nywele.....unajua maisha yako yote umekuwa na manywele lundo. Uwingi wa nywele hubadilika hasa baada ya kuzaa, mabadiliko ya homono na kadhalika.
Sasa kwasababu umekuwa ukijiongelea(mie)kama mtu usie na uhaba wa nywele ukweli huo hubaki kichwani na hata uhaba unapokukabili bado utaendelea kuamini kuwa wewe ni manywele person.
Kuna siku nikawa nazungumzia Nyusi(ninazo za kumwaga.....well used to)....kwanini watu wanachora badala ya kujazilizia palipopungua. Kwa kujiamini(bila kujua) kabisa nikasema bora mie nina manyusi mengi....
......asali wa Moyo akasema kwa upole na huruma "mbona mie sizioni hizo nyusi zako nyingi".....nikamkata jicho hilo(baadae kisirisiri nikaenda kujiangalia). Daaah! Manyusi yangu yamepururuka lini lakini? Nkajiuliza.
Kipindi hicho nilikuwa nimepoteza nywele za kutosha kichwani (postnatal shedding) na sikuwa nikijiangalia kwenye kioo(nina kichanga muda nitoe wapi).
Kabla hujalitoa mdomoni pata second opinion kutoka kwa mtu unaemuamini kukupa ukweli hata kama unauma. Ahsante kwa kuichagua Blog hii.
Babai.
Comments