Sunday, 28 June 2015

Usilaumu kabla hujajua kwanini

Aah kuumwa aka holiday(mpaka niumwe ndio napumzika kuwa Mama a little).......jikapata nafasi ya kusoma article moja (ndefu ka kitabu)kuhusu Wabritishi wanaojiunga na ISis.


Nimepata mwanga mpya kuhusu hao jamaa na yote wayafanyayo. Imeeleza kwa kifupi tu kuwa Kuishi Nchi za Kimagharibi kunawafanya wajihisi kuwa sio Waislam enough.Ukifuatilia hnagundua kuwa ni kweli kwasababu  Muislam wa kweli hawezi kuishi Nchi kama Uingereza.....wanaoishi humo ni wale wanaotaka kuubadilisha Uislamu ili kwenda na wakati, kwamba wanataka kuwa Waislamu wa kisasa.Vijana hao wanadai kuwa Wamekuzwa Kiislamu na Wazazo wao lakini baada ya kuwa watu wazima wamegundua kuwa Wazazi wao wamekosea kwa kuja kuishi Uingereza.Kuishi Uingereza kunamfanya Muislamu kutokuwa Muislamu kwasababu ya Mazingira, Utamaduni,Ubaguzi na kufunga Masaa 19 mwezi wa Ramadhani(nimeongezea hihihi).


Mpaka leo sielewi ni kwanini hasa Waislamu hukimbilia Nchi za Kimagharibi(za Makafiri) na kuacha Nchi za Kiislamu tulivu?Au kama wasemavyo wao kuwa Muislamu kula Mali ya Kafiri ni Halal....Nenda google kisha weka "the secret of isis brides the guardian" ukajifunze mawili-matatu.

Babai.

No comments: