...isipokuwa mimi! Kumbuka kuwa sehemu kubwa ya haya mambo ni uzoefu wangu binafsi ambao unaweza kukutokea wewe pia, sasa ikikutokea usishangae na kudhani kuna "uchawi" na isipokutokea haina maana kuwa una tatizo. Mimba sio lelemama kama ambavyo baadhi ya watu hasa wa kiafrika wavyojiaminisha. Kila mimba unayoshika ni tofauti(uzoefu tofauti) japokuwa mimba zote zinaongeza uwezekano wa Maradhi ya kudumu kwako sasa au huko mbele. Jinsi ambavyo unashika mimba mara nyingi ndivyo ambavyo unajiongezea matatizo pale utakapofikiwa umri mkubwa. Imagine "kuhisi" kichefuchefu masaa yote 24 kwa miezi 4, kutokuwa na nguvu mwilini, maumivu ya viungo na msuli, kichwa, mgongo, nyonga na kinena, ukubwa wa matiti yanayouma na yamekuwa makubwa yanafika shingoni na unashindwa kupumua....hapo sijazungumzia Uchungu wa kuzaaa, hofu na uhai wako na mtoto na kuzaa kwenyewe. Oh halafu kuna ile "maziwa kuja", ugumu wa kunyinyesha na kukesha na kichanga kwa miezi mingine 4.....ha