...isipokuwa mimi!
Kumbuka kuwa sehemu kubwa ya haya mambo ni uzoefu wangu binafsi ambao unaweza kukutokea wewe pia, sasa ikikutokea usishangae na kudhani kuna "uchawi" na isipokutokea haina maana kuwa una tatizo.
Mimba sio lelemama kama ambavyo baadhi ya watu hasa wa kiafrika wavyojiaminisha. Kila mimba unayoshika ni tofauti(uzoefu tofauti) japokuwa mimba zote zinaongeza uwezekano wa Maradhi ya kudumu kwako sasa au huko mbele. Jinsi ambavyo unashika mimba mara nyingi ndivyo ambavyo unajiongezea matatizo pale utakapofikiwa umri mkubwa.
Imagine "kuhisi" kichefuchefu masaa yote 24 kwa miezi 4, kutokuwa na nguvu mwilini, maumivu ya viungo na msuli, kichwa, mgongo, nyonga na kinena, ukubwa wa matiti yanayouma na yamekuwa makubwa yanafika shingoni na unashindwa kupumua....hapo sijazungumzia Uchungu wa kuzaaa, hofu na uhai wako na mtoto na kuzaa kwenyewe.
Oh halafu kuna ile "maziwa kuja", ugumu wa kunyinyesha na kukesha na kichanga kwa miezi mingine 4.....halafu kuna M-baba anasema "wanawake wa bongo wanadeka sana wakiwa na mimba". anyway hii ni topic inayojitegemea, tuanze na namba Mosi;
-Mimba inaharibu afya yako na uwezekano wa kuwa na maradhi ya kudumu ambayo hujawahi kuwa nayo kabla ni mkubwa(kwamba Mimba inaweza kuwa sababu ukawa na afya mbovu). Ndio maana ni muhimu kutoa mwili wako na viungo vya uzazi kwa Mwanaume ambae ni Mume wako na anaestahili kujitoa Mhanga kwako kwa ajili ya kumpa familia Mpya.
Pili;-Ni bahati kuvuka miezi yote na hatimae kujifungua salama na kupita Wiki 12 za mwanzo bila maambukizo(na hata kifo) kwako na kwa mtoto baada ya kujifungua.
Tatu;- Ukubwa na nguvu ya Moyo wako unaongezeka, sasa kama una matatizo ya Moyo au tayari ni Chibonge au mtu mzima (miaka 46+)ni muhimu kutambua faida na hasara kwako linapokuja suala la kushika Mimba.
Nne;- Ukubwa wa miguu(vikanyagio huongezeka kwa size 1), wewe ulidhani ni matiti, pua, makalio na tumbo tu eti?
Tano. Kipindi mimba ni changa unajikuta ukihitaji tendo la ndoa mara kwa mara na kila baada ya tendo unahisi kinyaa na harufu ya "ndoa" kati ya Manii ya mumeo na Utoko wako ndio balaa inazidi. Ukisha jiswafi, utahisi kutaka tena Tendo...hii itaendelea kwa miezi yote tisa(kumi).
Sita;-Uwingi wa Utoko unaongezeka hata ujiswafi(shije) na ni kero kubwa mno. Ila kitibabu wanashauri usijiswafi mara nyingi ili kuepuka maambukizo Ukeni na hata kumfikia mtoto. Hivyo jiswafi mara mbili kwa siku.
Saba;- Ngozi yako inakuwa "sensitive to the touch" na sio kwa uzuri....inakuwa kama inauma hivi...iwe mikono ya mumeo, Daktari, Mkunga, maji wakati wa kuoga au nguo uvaazo.
Je umewahi pitia uzoefu tofauti na ungependa wengine wafahamu? Naomba unisimulie.
Mpaka siku ingine, Bai.
Comments