Skip to main content

Posts

Showing posts with the label maisha ya familia

Jinsi ya kurudisha Furaha Ndoani 2...

  Yafuatayo yatakusaidia kurudisha furaha kwenye Ndoa yenu ikiwa mtashirikiana na kuyafanyia kazi. Yote haya mmeishawahi kuyaishi hivyo hakuna ugumu/jipya, sema tu mmezeoana so mnayachukulia kawaida, kwamba hayana "maana/umuhimu" kwa sasa.   -Wote; Acha yaliyopita huko huko yalikopita, kamwe usiayarudishe tena kwasabau tu unataka kushinda mabishano au unataka kumkumbusha mwenzio ni kiasi gani umemsamehe au namna gani alikuwa bwege hapo zamani za kale ili kumshusha na kumuumiza hisia zake(huo ni utoto).   -Wote; Unakumbuka enzi zile kabla hamjawa wazazi? Mlikuwa lovers, natambua hii inaweza kuwa ngumu hasa kwa sisi wanawake(wake)kwasababu katika haki halisi tumebadilika kiakili, kimwili na kiafya. Uzazi ni kujitolea mhanga, uzazi unakuja na trauma sio kimwili tu bali kiakili, Uzazi unabadilisha namna unamuona mumeo sio kwamba anapoteza umuhimu bali unahisi hakuhitaji tena kwasababu kuna kichanga.   Waume zetu mpo vile vile kimwili kwasababu hamkubeba mimba na hamk

Kutoa ushauri wa Mapenzi, Ngono na Ndoa...Elimu, Uzoefu na Mazingira vinatosha?

  Za leo? Muibuko wa Podcast za wakaka na dada wajuzi wa maisha ya Ndoa zimekuwa nyingi na karibu wote (kutokana na uchunguzi nilioufanya) hawajawahi kuishi Maisha ya ndoa, lakini wanashauri wenzao(hasa wanawake) namna ya kuishi na Mume. Bila kutilia maanani kywa kuna tofauti kubwa sana kati ya kuishi na mpenzi na kuishi na mke/Mume.   Binafsi sidhani kuwa unahitaji Elimu….kwasababu matatizo hayo hayafanani   kwa ukaribu na hakuna dalili zinazofanana kama vile Magonjwa, matatizo ya kimaisha, afya ya akili. Mapenzi na ndoa yameegemea zaidi kwenye aina ya wahusika(muonekano/kipato), malezi, mazingira na jinsi   mhusika alivyo umbwa/zaliwa(japokuwa tunazaliwa na ubongo mtupu)…tuegemee kwenye Malezi na mazingira, maana suala la kipato na muonekano ni la majaaliwa. Pamoja na kusema hivyo Elimu kuhusu Tabia za binadamu na jinsi ubongo unavyofanya kazi inaweza ikasaidia Zaidi, ila kumbuka Ubongo ni complex na “chemical” zake zinaweza kutofautiana   kutoka kwa mtu na mtu na kutoa matokeo t

Mambo 10 kuhusu Ujauzito hakuna mtu atakuambia....

 ...isipokuwa mimi! Kumbuka kuwa sehemu kubwa ya haya mambo ni uzoefu wangu binafsi ambao unaweza kukutokea wewe pia, sasa ikikutokea usishangae na kudhani kuna "uchawi" na isipokutokea haina maana kuwa una tatizo. Mimba sio lelemama kama ambavyo baadhi ya watu hasa wa kiafrika wavyojiaminisha. Kila mimba unayoshika ni tofauti(uzoefu tofauti) japokuwa mimba zote zinaongeza uwezekano wa Maradhi ya kudumu kwako sasa au huko mbele. Jinsi ambavyo unashika mimba mara nyingi ndivyo ambavyo unajiongezea matatizo pale utakapofikiwa umri mkubwa.   Imagine "kuhisi" kichefuchefu masaa yote 24 kwa miezi 4, kutokuwa na nguvu mwilini, maumivu ya viungo na msuli, kichwa, mgongo, nyonga na kinena, ukubwa wa matiti yanayouma na yamekuwa makubwa yanafika shingoni na unashindwa kupumua....hapo sijazungumzia Uchungu wa kuzaaa, hofu na uhai wako na mtoto na kuzaa kwenyewe.  Oh halafu kuna ile "maziwa kuja", ugumu wa kunyinyesha na kukesha na kichanga kwa miezi mingine 4.....ha