Za leo?
Muibuko wa
Podcast za wakaka na dada wajuzi wa maisha ya Ndoa zimekuwa nyingi na karibu wote (kutokana
na uchunguzi nilioufanya) hawajawahi kuishi Maisha
ya ndoa, lakini wanashauri wenzao(hasa wanawake) namna ya kuishi na Mume. Bila kutilia maanani kywa kuna tofauti kubwa sana kati ya kuishi na mpenzi na kuishi na mke/Mume.
Binafsi
sidhani kuwa unahitaji Elimu….kwasababu matatizo hayo hayafanani kwa ukaribu na hakuna dalili zinazofanana kama
vile Magonjwa, matatizo ya kimaisha, afya ya akili. Mapenzi na ndoa yameegemea zaidi
kwenye aina ya wahusika(muonekano/kipato), malezi, mazingira na jinsi mhusika alivyo umbwa/zaliwa(japokuwa
tunazaliwa na ubongo mtupu)…tuegemee kwenye Malezi na mazingira, maana suala la
kipato na muonekano ni la majaaliwa.
Pamoja na
kusema hivyo Elimu kuhusu Tabia za binadamu na jinsi ubongo unavyofanya kazi
inaweza ikasaidia Zaidi, ila kumbuka Ubongo ni complex na “chemical” zake
zinaweza kutofautiana kutoka kwa mtu na
mtu na kutoa matokeo tofauti kulingana na tabia(mazao ya malezi) na Uzoefu(mazao
ya mazingira) ya mhusika.
Enzi za
miaka ya 80(kabla hujanijaji kuwa nimezeeka which I am ila enzi hizo nilikuwa mtoto) wazee walitumika kama
watoa ushauri kwasababu ya uzoefu wao wa Maisha japokuwa maelekezo yao mengi
yalifanana na kumkandamzia mwanamke Zaidi. Hawakujali au walikuwa hawajui kuwa
kila binadamu ni tofauti sio tu kimalezi bali pia kimazingira.
Nimeanza
kutoa ushauri kwa watu nikiwa a teen(miaka ya 90) tena bila uzoefu wa ngono wala Maisha ya
kimapenzi na bila internet. Nakumbuka siku moja kuna Dada alinijia na kuniuliza
kuwa “hivi mwanaume akikuingilia halafu akagundua upo hedhini,
akasinyaa…inamaana hakupendi”...nikamwambia, Hapana huenda damu ilikuwa nyingi
ukeni hivyo akashindwa sababu ya kinyaa(kumbuka kibongo bongo damu ya hedhi inachukuliwa
kama uchafu).
Kama Binti
wa kwanza kwenye familia, nilipata bahati ya kupewa mafunzo ya ziada nje ya
shule(kuniandaa kwa ajili ya Maisha ya Ndoa) na hivyo nilijuwa mambo mengi
kuhusu mapenzi, ndoa na ngono kabla sijashiriki kwasababu ya ulazima wa kupewa
Elimu ya awali(kufundwa)iliyotolewa na watu ambao walikua kwenye mazingira ya
“kizamani” miaka ya 1900s kabla ya 1950s si unajua enzi hizo wanawake walikuwa
hawapaswi kusoma….so ukibalehe tu, unaolewa.
Nilipoanza
kazi kwenye Kampuni ya Media, niligundua kuwa washauri wengi kuhusu mapenzi
kwenye magazeti walikuwa wanaume wakitumia majina ya kike ili kufikisha ujumbe
kuhusu uzoefu wa mwanake. Nilishangaa, nikacheka na kikakasirika. Hasira na Mshangao ule ndio ukazaa Dinahicious Blog, nikiwa tayari nina uzoefu na Muda.
Pamoja na
kusema hayo, sidhani kama ni sahihi kushauri mtu kuhusu Maisha ya ndoa kama
hujawahi kuishi kwenye Ndoa. Ndoa ni mtindo wa Maisha (ndio mnaita life style?)
ambao umekubaliwa na ninyi wawili, Mungu na Serikali. Makubaliano hayo yana
sheria na miiko yake ili kuboresha Maisha ya ndoa(basic na kila mtu anatakiwa
kujua na kufuata) na kujenga familia. Vile vile kuna sheria, makubaliano na
mipaka wanandoa wanajiwekea na kukubaliana wenyewe ili kuboresha amani na kufurahia ndoa yao
kulingana na uzoefu wa makosa waliopitia wakiwa ndoani humo.
Nimeongea mengi
yasiyo na maana eti? ni matumaini yangu kuwa sijakuchanganya, nia yangu ni
kutaka utambue kuwa kutoa ushuri mzuri sio lazima kusomea japokuwa uzoefu
utasaidia zaidi kuaminika na hivyo watu kuchukua mawili-matatu na kuyatumia na
kuacha 280 yasiyowafaa.
Mwisho
kabisa napenda ukumbuke kuwa makini na unayosikiliza na kusoma mitandaoni, baadhi
ya watoa ushauri wanataka ufanye kama walivyofanya wao ili ukosee wafurahi au
kama vile wangependa ufanye hayo kwasababu wangependa wenza wao wafanye hivyo
huko mbele…hivyo hakikisha unaangalia ni nani hasa anatoa Ushauri….jiulize je
anatoa ushauri huu kwasababu aliumizwa?
Je, ni
kwasababu Mama na baba yake walikuwa na Ndoa mbovu?
Je,
anachukia wanawake kwasababu Mama yake hakuwa mwema?
Je, anaongea
yote hayo ili kupata “shock value” na hivyo kupata “click”, “views” nyingi na
kuongeza kipato(asilimia 99% wanasaka kipato)?
Nikutakie
siku njema.
Baibaiiii.
Comments