Skip to main content

Posts

Showing posts with the label Ndoa nzuri

Kutoa ushauri wa Mapenzi, Ngono na Ndoa...Elimu, Uzoefu na Mazingira vinatosha?

  Za leo? Muibuko wa Podcast za wakaka na dada wajuzi wa maisha ya Ndoa zimekuwa nyingi na karibu wote (kutokana na uchunguzi nilioufanya) hawajawahi kuishi Maisha ya ndoa, lakini wanashauri wenzao(hasa wanawake) namna ya kuishi na Mume. Bila kutilia maanani kywa kuna tofauti kubwa sana kati ya kuishi na mpenzi na kuishi na mke/Mume.   Binafsi sidhani kuwa unahitaji Elimu….kwasababu matatizo hayo hayafanani   kwa ukaribu na hakuna dalili zinazofanana kama vile Magonjwa, matatizo ya kimaisha, afya ya akili. Mapenzi na ndoa yameegemea zaidi kwenye aina ya wahusika(muonekano/kipato), malezi, mazingira na jinsi   mhusika alivyo umbwa/zaliwa(japokuwa tunazaliwa na ubongo mtupu)…tuegemee kwenye Malezi na mazingira, maana suala la kipato na muonekano ni la majaaliwa. Pamoja na kusema hivyo Elimu kuhusu Tabia za binadamu na jinsi ubongo unavyofanya kazi inaweza ikasaidia Zaidi, ila kumbuka Ubongo ni complex na “chemical” zake zinaweza kutofautiana   kutoka kwa mtu na mtu na kutoa matokeo t

Mambo 7 Mumeo angependa umfanyie, ila...

...anaogopa kukuambia. Heri ya Mwaka mpya 2023 kwanza, leo google wamenitumia "data" bana, wanasema mwezi wa january kumekuwa na watu Laki nane na Eflu 11(8.11K) wametembelea Blog hii....nikasema Mayooo wane nimezeeka! nilikuwa napata idadi hiyo kwa Siku😅anyways, kama wewe ni mmoja wao basi nasema ahsante sana. Naendeleaje bila twita kwa Miezi 7? Vema kabisa, ahsante kwa kujali. nimegundua kuwa nina Muda mwingi sana wa kufanya mambo mengine muhimu kwa ajili ya afya ya Akili yangu. Ila baada ya kugusa miezi 4 hali ilianza kuwa ngumu nikawa nawakumbuka wote ambao tulikuwa tunabadilishana twiti mara kwa mara nikataka kushusha App, nikapata nguvu za kughaili, nikashida.  Vipi Mumeo na wanenu 3? Bado tumeshikiliana kwa mapenzi ya dhati, wanetu wanaendelea vema pia shukurani. Sema nini gharama na uhitaji wa kugawa "attention" kwa individual's umri na mahitaji yao Kiakili, Elimu, Malezi na "daily Activities" yameongezeka hyuuu!! Ila kwenye mambo mengine wan