Za leo? Muibuko wa Podcast za wakaka na dada wajuzi wa maisha ya Ndoa zimekuwa nyingi na karibu wote (kutokana na uchunguzi nilioufanya) hawajawahi kuishi Maisha ya ndoa, lakini wanashauri wenzao(hasa wanawake) namna ya kuishi na Mume. Bila kutilia maanani kywa kuna tofauti kubwa sana kati ya kuishi na mpenzi na kuishi na mke/Mume. Binafsi sidhani kuwa unahitaji Elimu….kwasababu matatizo hayo hayafanani kwa ukaribu na hakuna dalili zinazofanana kama vile Magonjwa, matatizo ya kimaisha, afya ya akili. Mapenzi na ndoa yameegemea zaidi kwenye aina ya wahusika(muonekano/kipato), malezi, mazingira na jinsi mhusika alivyo umbwa/zaliwa(japokuwa tunazaliwa na ubongo mtupu)…tuegemee kwenye Malezi na mazingira, maana suala la kipato na muonekano ni la majaaliwa. Pamoja na kusema hivyo Elimu kuhusu Tabia za binadamu na jinsi ubongo unavyofanya kazi inaweza ikasaidia Zaidi, ila kumbuka Ubongo ni complex na “chemical” zake zinaweza kutofautiana kutoka kwa mtu na mtu na kutoa matokeo t