Skip to main content

How is life as a mother to a third child (Maisha yakoje kama mama kwa mtoto wa Tatu)?

  Hello, jambo?

Baada ya  kichwa cha habari hapo basi umejisema " watu wana watoto 7 na huoni wakitusimulia kuhusu maisha yao", labda hawana muda kama mimi au dada wa kazi ndio anawalea(atakusimulia aliyosimuliwa na dada wa kazi ambae ndio mlezi wa watoto)? achana na hili.


Kiujumla maisha kama full time mother kwa watoto 3 chini ya miaka 15 ni magumu kwasababu watoto bado wanakutegemea kwa kiasi kikubwa  ila tegemeo ni tofauti na walivyokuwa wadogo(chini ya miaka 5). Pamoja na ugumu huo bado ukiwaangalia unahisi baraka ya kupata nafasi ya kulea, kukuza, kulemikisha na ku-shape vema wanadamu wengine kwa ajili ya manufaa ya Jamii.


Wanao wanapokuwa nje ya nyumbani na wanaonyesha tabia njema, wasikivu, wanajiamini(sio kupita kiasi) na wenye wema ni wazi kuwa wanafanya maisha ya watu wengine kama vile walimu, marafiki zao kuwa rahisi na pengine yenye "furaha" na hata kuwafanya waendelee kutaka kuwa marafiki zao au (walimu) kutokuwa na hasira(maana kazi yao ni kama yangu ila kwa watoto ambao sio wao).


Majuzi kati nimeona video(si amini watu bado wana-over share 2023) mbali mbali za wanawake wakilalamika na wengine kulia kuwa wanajuta kuzaa(kuwa mama) sababu watoto wao wanawajaribu....mmoja akadai Binti yake ni miaka 11 na nahisi kuwa kuna wakati huwa anamjaribu makusudi! Nkajisema miaka 11 ni mtoto of coz atakujaribu mara kibao tu kama vile alipokuwa na miaka 2 na nusu. Unategemea mtoto wa miaka 11 awe rafiki yako? ni mtoto anajaribu kuona Mipaka na sheria ulizoziweka bado zinafanya kazi au la! Sasa kama hukuweka mipaka na Sheria tangu alipokuwa mdogo unalo na utalibeba.



Ngoja na mimi ni-ovashee kidogo, nikilinganisha na wanangu wa 2 kwa kwanza, huyu wa tatu anaonekana anajua mambo mengi katika umri mdogo(ana miaka 3), anajieleza vema, pia anatumia maneno makubwa ambayo mimi mswahili nilikuwa siwezi kuyatamka nikiwa na miaka 25 na wenzake walianza baada ya kufika darasa la 3. 


Hii hana maana kuwa  ni "Jiniasi" bali ni kwasababu amewakuta wenzake wakiongea "kikubwa" hivyo hana muda wa kujifunza maneno ya kawaida ya kitoto.Hivyo kwa upanade mwingine nimesaidiwa kwenye kumfunza namna ya kuzungumza/tamka maneno kama nilivyowafunza wenzake kabla yake. Faida ya kwanza.


Faida ya pili ni kwamba nime-relax zaidi kwenye kumlea huyu mtoto wa tatu kwasababu tayari nimelea na kukuza Kaka na dada yake, nina uzoefu wa kutosha. safari hii sikuhitaji vitabu kama nilivyokuwa 1st  and 2nd time mother. Utauliza..."Dada Di ulihitaji vitabu kulea wanao?" Ndio...well nadhani kila 1st time mother nchi hii anapewa kitabu mara tu anapo-report kuwa ni mjamzito mapka kujifungua na ukijifungua unabebesha tabu lingine la kuanzia wiki 1 mpaka miaka 2. Vilinisaidia japo havikuniondolea uoaga wa kufanya makosa na hivyo niliendelea kuwa makini kupita kiasi which sio nzuri sana kwasababu ilinifanya niwe control freak(hakuna anaeza fanya kazi bora zaidi yangu, watakosea na kuumiza mtoto).


Faida ya tatu ni kila mtu familiani anataka kucheza nae, kusaidia kumbadilisha nguo kila anapojichafua na hivyo mie kupata muda wa kufanya mambo yao mengine(kazi zangu za kimama na zile za Mke wa nyumbani).


Kwenye kila kitu kuna faida na hasara zake, zifuatazo ni kinyume cha faida; Mosi, mtoto wa tatu anakua na kuanza kujitegemea haraka kwasababu anataka ku-catch up na wenzake ambao ni wakubwa na hiyo kama wazazi, hasa mama unakosa kufaidi ile "stage" ya utoto wake. Ni kama vile kazaliwa kavuka u-toddler na kuwa school kid....hakuna u-preschooler hapa.


Pili, kama wazazi mnahitaji kuwaelimisha watoto wakubwa namna gani mdogo wao bado ni "a baby", kwa vile tu anaongea kwa kiwango chao hainamaana akili na uelewa wake umekuwa kwa kiwango walichofikia. Bado tinairudia hii kila mara mtoto wa tatu anapishana na wakubwa zake na wao kum-treat kama vile ana miaka 7 na sio miaka 3. Hii inachosha sana akili na koo hasa kwa mimi mama wa nyumbani.


Tatu, Mashindano ya sanamu(ndio toys right?), mtoto wa kwanza na wapili hawahitaji kucheza na sanamu kama mwenzao mdogo, Wanacheza games na sports....sasa kila mara ukimnunulia sanamu, wakubwa wanadhani kuwa mnampendelea kwasababu wao hawapati chochote.....hapo unaanza "lecture" ya kwanini mdogo wao ananunuliwa toys, na kuonyesha picha zao ktk umri wa mdogo wao na kuona masanamu waliyokuwa nayo. Imagine kila ukinunua a toy unanunua game cards, Chuuu, mwana mayu!!


Nne, nikiwa na wanangu mtaani utasikia watu wakinambia "mikono yako are full",  na that they hope  the parents (of my own children imagine) are paying me good"...Excuse me? 


Pamoja na changamoto za  kawaida kama mama kwa mtoto mdogo yeyote bado maisha kama mama kwa mtoto wa tatu ni nafuu kuliko nilivyokuwa mama kwa watoto wawili. Hii  nahisi ni kwazababu walifuatana kwa karibu, kuna nafasi kubwa sana kutoka mtoto wa pili na wa tatu. 


Huwezi kufanya uamuzi wa kuleta mwanadamu duniani halafu baadae useme "najuta" kukuzaa....juta kukubali kushika Mimba, mtoto hakuomba kuzaliwa na wewe, hivyo ni jukumu lako kukabiliana na lolote analohitaji mtoto kiakili, kisaikolojia, kiuchumi nakiafya. Halafu acheni ku-over share.


Mpaka wiki ijayo, bai baiiiiiii.

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao