Pamoja na kusema hivyo haina maana kuwa Dini ndio kimbilio kwasababu ukizidisha huko Dinini pia unaweza kuongeza viungo kwenye matatizo yako ya akili au kuongezea mengine. Unapokuwa unafuata Imani ya Dini (Traditional Churches na Uislamu, hao matawi ya ukristo wa kisasa aka MATAPELI mie siwatambui) inakusaidia kuishi kwa heshima na kufuata princimples zake, unajua nini chakufanya(unamkimbilia Mungu) unapopata matatizo mfano kupoteza kazi, migogoro kwenye urafiki, wazazi, ndoa, ndugu au hata pale unapoyumba kiimani. Sio tu kwamba unakuwa na kimbilio (Mungu) bali pia unakuwa na Community kutokana na Asilia yako(Kabila) ambayo kwa kiasi kikubwa mnakuwa mnajadili masuala mbali mbali ya kimaisha na mnakuwa na activities hata kama ni mara moja kwa Mwaka, mnakuwa karibu kwavile mnamisingi inayofanana, mnaiheshimu na hivyo inakuwa rahisi kuepuka “Drama” ambazo ni chachu ya matatizo ya Akili. Kutokana na muibuko wa social media, kumekuwa na watu wakipeana mioyo au kufundishana