Pamoja na kusema hivyo haina maana kuwa Dini ndio kimbilio
kwasababu ukizidisha huko Dinini pia unaweza kuongeza viungo kwenye matatizo
yako ya akili au kuongezea mengine. Unapokuwa unafuata Imani ya Dini (Traditional
Churches na Uislamu, hao matawi ya ukristo wa kisasa aka MATAPELI mie
siwatambui) inakusaidia kuishi kwa heshima na kufuata princimples zake, unajua
nini chakufanya(unamkimbilia Mungu) unapopata matatizo mfano kupoteza kazi, migogoro kwenye urafiki, wazazi, ndoa, ndugu au hata pale unapoyumba kiimani.
Sio tu kwamba unakuwa na kimbilio (Mungu) bali pia unakuwa
na Community kutokana na Asilia yako(Kabila) ambayo kwa kiasi kikubwa mnakuwa
mnajadili masuala mbali mbali ya kimaisha na mnakuwa na activities hata kama ni
mara moja kwa Mwaka, mnakuwa karibu kwavile mnamisingi inayofanana, mnaiheshimu na hivyo inakuwa
rahisi kuepuka “Drama” ambazo ni chachu ya matatizo ya Akili.
Kama unaishi nyumbani(Tanzania) huenda usihisi upweke na
hata kuhitaji sense of community kwasababu tayari upo karibu na ndugu na jamaa,
kama sio wa Damu kuna wale wa Kikabila ambao mna-share values zilezile kwasababu.
Miezi kadhaa nilikuwa kwenye Semina kuhusu Matitizo ya Akili,
waandaaji wakawa wanauliza ni vitu gani vinasababisha matatizo ya Akili? Watu mbali
mbali wakawa wanajibu,kuwa ni Mazingira, Urithi, Unyanyaswaji kiakili, kihisia na
kimwili katka umri mdogo, Matukio Hasi ya kimaisha (Vifo na Uzazi) kupoteza kazi/Ndoa na Umasikini.
Waliposema umasikini, nikashtuka na kama kawaida yangu nikabisha
kuwa Umasikini peke yake hausababishi
matatizo ya Akili isipokuwa ukosefu wa Imani ya Dini na Community, nikaambiwa
nielezee how? Nikawaambia nilipozaliwa (Tanzania) na kupata elimu yangu ya
awali, kuna masikini mkuu na wengi hawasumbuliwi na matitizo ya Akili kama
watu wa nchi hii ambao katika hali halisi sio masikini in comparison. Watu wa
Nchi za Magharibi wameacha kumuamini Mungu(hawana principles wala values) na wanalea Watoto
wao kiholela bila Misingi, Mipaka wala Values za kufuata/simamia.
Ukiangalia Tiba ya Matatizo mbalimbali ya akili moja wapo ni
kujiunga na Vikundi vya watu ambao wanamatatizo kama yako, hii haina tofauti na nilichosema hapo
juu kuhusu umuhimu wa kuwa na “sense of community” iwe Dini au Kabila au vyote(ila
usipitilize).
Siku hizi watoto wanakua tu
kama Miti Michakani huku wakiamini kuwa wao kama wao wanauwezo wa kufanya
chochote watakacho na hata kuvuka mipaka bila kujua wameivuka na hawajui wapi
pa kukimbilia Zaidi ya Wanadamu wenzao(Madaktari na wataalamu wengine wa
matatizo ya Akili) ili kupata msaada wa kiimani. Mtoto wa miaka 8 anakua
akitegemea madawa kurekebisha ubongo wake(dawa za anxiety au za kuzuia mimba zote zina athiri Ubongo), huyu mwanadamu akifika miaka 20
atakuwa hajijui kwasababu kwa miaka 12 artificial brain chemicals zimekuwa
zikirekebisha natural brain chemicals alizozaliwa nazo. Siku akichoka kutumia
dawa ili awe kama rafiki zake ambao hawatumii midawa daily…anakuwa mwehu na
kusababisha madhara kwa wengine!
Natambua kuwa watu nchi za Afrika wana matatizo ya akili
lakini sio kwa kiasi kukubwa sana kama huku nilipo hasa kwa watoto, Watoto wengine
wanahitaji Upendo, wanahitaji wazazi wao karibu na attention na sio Anti-depressant
au anti-Anxiety. Lakini kwasababu siku hizi wazazi wote mpo busy Kazini na wengine mkaamua kuwa
single parent by choice, muda wako kama mzazi kutoa attention/kulea na kupenda
kwa vitendo mtoto/Kijana/Binti unakuwa haupatikani kirahisi. Hii ina madhara makubwa sana kwa Mtoto ambae anakua na baadae kuwa mtumzima mwenye matatizo ya Aikili.
Siungi mkono watu waendelee kuishi kimasikini, nilichojaribu
kusema ni kuwa Umasikini pekee sio sababu ya kuwa na matatizo ya Akili,
ukizingatia Masikini wa Nchi hii ni Mwananchi wa kipato cha kati Tanzania…Hata
hivyo, nikutakie siku njema.
Comments