...ndio mnaita podcasts? wameharibu youtube eti, au nimezeeka niachane nayo kama nilivyoiacha twita? Anyways, hujambo? Unaendeleaje na u-pre-menopause?
Kama binadamu hakika kuna vitu vinakukera, binafsi nakwerwa na sehemu kubwa ya jamii ya online, hasa mamilionea na wamarekani weusi wanaoijua Afrika na kacha zake zote (nchi 57?) baada ya kwenda Ghana kwa wiki moja wa youtube na mi-microphone yao makubwa ka' wapo Mawingu FM. Halafu usinikumbushe wale wanajipanga kwenye vibox(zoom meetings) wanaanza kubishana oh my days.,,,ukute ni wivu wangu tu, maana wanangu wakienda shule na Baba yako Kazini nabaki hapa sina hili wala lile.
Ukiachana na hao kuna wale young single men and women wanashauri/fundisha wenzao namna ya kuishi maisha ya ndoa(Well I did that when I was younger but kama unakumbuka nilishauri kuhusu mahusino na ngono nilikuwa in one na was doing it). Najua unatambua kua sio tu Ndoa ni tofauti na maisha ya ndoa, pia Ndoa sio mahusiano japokuwa mahusiano ni sehemu ya ndoa. NO? Sawa bana. By the path Dinahicious imerudi hewani jana.
Baada ya hao, kuna wale Wabaguzi ambao ni weusi, sikuwahi kuamini kuwa watu weusi ni wabaguzi na hawezi kuwa wababguzi kwasababu hawamiliki Uchumi kama Bazungu, mapaka nilipoanza kuwafuatailia Black american, kabla hawajawa ADOS na baadae AFB(confused na identifications).....tangu awali nilijua Wamarekani weusi hawatupendi Waafrika, ila aisee, jamaa wabaguzi Mzungu haoni ndani, na hakuna mtu anawashughulikia kwa kuogopa kuitwa mbaguzi.
Halafu hehehehehee kuna Malaya na wauza ngono wa kike na kiume na ma-microphone yao makubwa wanafunza wanaume namna ya kupata wanawake/wanaume. Tubaki hapa, kuna wale wazee kama mimi hapa wameoa/olewa miaka ya 90s au early 200s huko(na ndio ilikuwa mara ya mwisho ku-date) leo hii wanafunza madogo on how to date? Maam/Sir, last time you dated was 1994....labda mtusimulie(historia hahahaha) jinsi mlivyokabiliana na maisha ya mapenzi/mahusiano bila internet/simu za viganjani!!
Pia wale wanaochukua kazi za wenzao na ku-react, yaani hakuna ubunifu (own/original thoughts) zaidi ya kukosoa/kukubaliana na kazi za wenzao, kutumia kazi ya mtu kama ushahidi au reference ya unachokizungumzia sio mbaya ila kuna mipaka. Kama ilivyokuwa twita kabla ya Musk(sijui ilivyo sasa), kwamba mtu anakuja na twiti yake halafu jamii nzima inaitumia hiyo twiti kama topic na kujifunza kwa ujumla. sio kila ukiingia twita/youtube kazi yako ku-quote na kujibu,,,,,huna original thoughts.
Kero yangu ya mwisho kabisa ni Mabilionea wanaofunza wenzao "how to" kwa kuwauzia e-books, kuwalazimisha wanunue sponsor's products au kujiunga kwenye Petrion au/na kuwa members kwenye channels zao kwa malipo.
Je una-share kero zangu au unazo zako tofauti? ongezea basi tucheke kwa pamoja.
Takuona wiki ijayo, bai baiii.
Comments