Skip to main content

Posts

Usinijaji....

....relax is a human nature! Tangu u-single mother umekuwa "fashion" vijana karibu wote wa late 20s na early 30s walishazaa huko nyuma, hivyo ni ngumu kweli kukutana na mtu ambae ni "m-clean" ka' wewe (hana mtoto/watoto). Shughuli inakuja kwa sie tuliozaa(Oa/Olewa) na Wanawake/Wanaume ambao washalizaaga "ujanani" huwa tunajajiwa sana yaani. Unaonekana "Mwizi" kwenye jamii na familia, hata mtoto aliezaliwa kabla wewe hujakutana na Baba/Mama yake uhisi kuwa wewe ndio sababu ya Baba/Mama yake kula Buti la pua ( I know how it feels cause I was a kid once). Unaenda mahali na Mumeo/Mkeo na tutoto twenu (bila yule wa kabla) watu wanawasonta-sonta (Shinganya Oyee!! Kusonta ni kukunyooshea kidole kama ulikuwa hujui)....anyway! Wengine bila haya wanaanza kuuliza "nanilihu na Mama/Baba yake hawajambo" mbele yako just to piss you off....Mindugu mingine Mikosi kweli!!? Inafikia mahali unajistuki

Kufananishwa/Linganishwa....

Jambo! "Baba yangu alikuwa bla bla bla kwanini wewe usi bla bla bla kama yeye" kaolewe na Baba'ko sasa (this apply to wakibaba pia, kaoe Mama yako sasa eti).... Kama tulivyozaliwa Nyakati, Siku na Dakika tofauti ndivyo ambavyo tunapaswa kuishi tofauti(na wazazi wetu). Utaishije maisha waliyoishi wazazi wako wakati wewe ni mtu tofauti na unaishi kwenye Nyakati tofauti na wao? Kuna zile "manners" nzuri ambazo ni muhimu maishani na kila familia inapaswa kuwafunza watoto, mfano Kusalimia, Kuomba, Ukarimu, Heshima, Kushukuru, Msamaha.... Kama utafananisha hizo hakunaga mashida, mengine yaliyobaki yaache yabaki huko huko yanako stahili. Ungependa kuwa au kuishi na mtu kama Baba/Mama yako? You need to go out a bit more rafiki.....by out I mean OUT OF YOUR COUNTRY!!! Kwaheri kwa sasa. Mapendo tele kwako...

Kujipendekeza Kipaji....

Helloooooo! Napenda kuandika mambo ambayo watu huogopa kuyasema lakini yanawakera...kwanini? Sababu sinywi Pombe hehehehe...! ....Kwa kawaida Ndugu wa mume hupaswa kuwa karibu na wewe (hata kwa ku-pretend) ili ujisikie umekaribishwa kwenye Ukoo eti...kwa Kacha yetu ya Kitanzania. Mwenyewe unajitahidi kuweka mawasiliano ya karibu....wao walaa(mpaka uwatafute)! Unajipa moyo labda wanashughuli nyingi na muda hawana, unasubiri siku mbili-miezi mitatu still Jiiiii....hee unaanza kujistukia, unataka kumuambia Mumeo lakini unaona noma. Maana wengine hawachelewi kukuambia "unataka kutugombanisha, we mwanamke tu....wale ndugu zangu"....so unaugulia Moyoni. Kujipendekeza mwisho mara 3(in my head), unajaribu kwa Mwaka mzima wao hawajitumi kukutafuta hata XMas to Xmas! Sina marafiki kwa ajili hiyo(sijui kujipendekeza, najaribu....usipoweka effort nafunga Ukurasa na songa mbele..... Unajiuliza nani atanizika "nikikufa

Kazi za watu...

Maoni ya Mhariri...siku hizi sote tunatoa Maoni on particular or similar issues....Teknolojia na Uhuru wa kujieleza/Changia utakacho au ulichokiona/shuhudia unaharibu kazi za watu. Mfano, kazi ya Uandishi wa Habari wa Magazeti na Radio....imeingiliwa na Blogs, Online Radios, Social Media na YouTube(is YouTube sosho Media pia?). Jamaa wanatumia Sosho Midia kama "chanzo cha uhakika" na wale Waandishi wavivu wa kukopi na kupesti ndio wamerahisishiwa kazi. Habari zenye Uzito ni zile za Uchunguzi....labda na mahojiano magumu ya Wanasiasa! Jana nipo YouTube (napenda Fashion Haul na beauty review....how sad!!?) nikakutana na Matangazo kutoka Kampuni moja kubwa ya Urembo....alietumiwa ni Vlogger na sio Model/Celeb kama nilivyozoea. Nkajisemea eeh Teknolojia imeharibu na kazi za Celebs na Model pia.....sio haki kabisa! ....Hebu ngoja kwanza! Hawa Vlogger ni real people wanatumia bidhaa na kuzi-review hivyo wao kutangaza bidhaa husika wana