Skip to main content

Posts

Weusi mzuri...

If you have to tell us then it isn't....Mambo vipi? Weusi wa Afrika tuna issues zetu ambazo zinasababishwa na Watawala wetu(Siasa)....ila Weusi wa Wamarekani wana issues vichwani mwao kuhusu Weusi wao, yaani wapo ka' Mikorosho vile. Ujue kunatofauti ya kujivunia ulivyo na kulazimisha watu wajue kuwa unajivunia ulivyo. Mf: Kuna ulazima gani wa kusema "mimi ni mweusi na ninajivunia" wakati tunakuona wewe ni mweusi, unajipenda, unapendeza na unafanya mambo yako kama watu wengine. Kwanini utulazimishe kutambua kuwa "unajivunia"? Mf wa pili; Kitu gani kinakufanya uweke "kichwa cha habari" cha video/picha na kusema "beautiful black baby"....kwani ukiandika "baby" au "beautiful baby" haileti maana au hakuna watoto weusi na wazuri isipokuwa huyo wako? Unatulazimisha kutambua kuwa unajivunia Weusi wako alright, lakini picha/video "unazipausha" ili zionekane na karan

Kumbukumbu...

Nimekaa hapa nakumbuka watu wote niliosoma nao Msingi na Sekondari kwa Majina yao yote Mawili(la mwanzo na la Mwisho).....nimeambulia kusisinzia. Darasa Moja tulikuwa. Wanafunzi 200na! Tuligawanywa katika Mikondo 5 yaani A-B-C-D-E-F....shule kubwa ka' Kijiji....hiyo Msingi. Sekondari hatukuwa wengi sana Mikondo ilikuwa Minne. Sasa mwanamke nkasema ngoja nipime uwezo wa akili yangu sehemu ya kutunza kumbukumbu....nimefeli yaani nimepoteza kumbukumbu hata Miaka 40 sijafika!. Nikajipa Moyo; labda niagize picha za enzi za shule ili nikiona sura zao niwakumbuke vema, lakini hata hivyo sikupiga picha na kila mtu niliesoma nae kwahiyo haitosaidia. Yaani ndio basi tena. Nimejisikia vibaya sana....yaani kupoteza kumbukumbu ya sehemu ya Maisha yako ndio inauma hivi?!!! Kama ulisoma na mimi na unanikumbuka eeh! Drop me a line. Babai... Mapendo tele kwako...

Msingi/Malezi bora...

Habari gani? Kuna watu walikosa Malezi(Msingi) bora utotoni, malezi bora sio kula vizuri, kuvaa vizuri na kusoma shule nzuri bali kulelewa katika Mazingira ya Heshima na Adabu (kwako na kwa watu wengine), Staa/Stara, Uvumilivu, Kuridhika, Kutokata tamaa, Utu na Haiba. Hivi majuzi nimekutana na mtu akaanza nipa stori za mambo na vitu Ghali anayomfanyia Ex wake....nadhani alitaka kufikisha ujumbe kuwa yeye ni mtu wa kujali sana na kutumia Mahela kwakwe sio tatizo. Kwa bahati mbaya alikuwa hajui kuwa mimi ni Mwanamke (a bit tofauti) sibabaiki na Mahela ya watu kwani naamini ninauwezo wa kutafuta na kupata zangu.....pamoja na kusema hivyo zawadi napokea hihihihihi! Stori zikaendelea huku nami (kama kawaida) nikiuliza maswali...."Kwanini unamhudumia Ex wakati una mwanamke mpya?"...."Kuna kitu unataka au unapata kutoka kwa Ex"..."Je, Ex ana siri zako nzito unaogopa atazitoa"? n.m(na mengineyo). Kabla hatujaagana chi