Skip to main content

Posts

Kizazi cha Miaka ya 90!

Na haraka zao!! Yaani wapo mbio-mbio tu japo mbio zao zinatofautiana.....kuna wale wa starehe(Now) na wa maisha yajayo(Future)!! Mdogo wangu wa Mwisho anatarajia kufunga ndoa hivi karibuni. Nilipopata habari za yeye Kuposwa nilipata hasira za ajabu! Nikabaki nalalamika "yaani mdogo wangu mdogo hivi anaolewa"...."Vipi huyo mwanaume akienda kumtesa"? "Kwanini asisubiri kidogo jamani akue (huku nalia) bado mdogoooooooo" she's 23yrs! Mama akaniuliza(Simuni), ningekupa taarifa kuwa anamimba au kazaa ugelia kiasi gani?!! Kabla sijajibu!! Asali wa Moyo nae akauliza swali hilo hilo(live).....nikasema but she's my little sister....can she just wait another 2yrs?!!! Anyway, ilinichukua mwezi Mzima kukubali kuwa my baby little sister-o anaenda kuolewa!! Sasa leo naongea nae, ananiambia "nipo site dada" Nkauliza Site ya maandalizi ya Ndoa? Akanijibu "Hapana Da Dinah, tunajenga"!!

Nimeachwa na Teknolojia...

Ah! Nimebanwa kweli siku mbili hizi....ila nafurahi kuwa nimepata muda wa kuongea na wewe kabla sijaenda kulala.....mmh! Tangu nimekuwa Mama wala hakuna kulala ni kujilaza tu. Kuna tuwimbo tuwili twa Ali Kiba tunanikuna kweli yaani "Mwana Daslama" na "Kimaso" ingekuwa zile Kanda za enzi ninge-rewind kwa Penseli mpaka Kanda ikatike....ujue kuna Wasanii wa Bongo Flava halafu kuna Ali Kiba(I just love that Kid). Achana na hili. Jana nikaenda Dukani kuangalia Simu....Teknolojia imenishinda au niseme tu imenipita! Simu yangu ya mwisho ilikuwa (usicheke) Blackberry Bold 9900, ikatumbukia chooni (umama siku za mwanzo uliniCost!!!). Siku naenda mtembeza mwanangu City center kwa mara ya kwanza si nilipanda Treni heheheheheeeeeeee mwanamke nashuka na "Pram" lenye Mwanangu obviously!!....nikaacha Hand bag kwenye Treni(walinirudishia though)! Turudi kwenye Teknolojia ya Simu, wala siamini kama nimekaa Miaka 3 bila

Mtu chake...

Kwa kawaida mimi sina tabia ya kuangalia watu ninapokuwa natembea na hata kama nimekaa mahali nitakuangalia kama nimependa ulichovaa....na kuangalia kwenyewe ni kwa Sekunde chache tu. Kuna watu wanajua kukodolea macho wenzao bila kupepesa! Yaani anakukazia macho mpaka unaona aibu kwa ajili yake! Ukitaka ugomvi na watoto wa London wale wa Uswahilini bana wakazie Macho hivyo....anakufuata na kukuuliza "what you looking at?" huku kashikilia Kisu! Kisu bit pale juu nimeongezea tu chumvi, ila kuna vipigo na vifo kadhaa vilitokea kutokana na mtu kumkodolea macho mwenzie. Stori time: Sasa jana tupo mtaani tunatembea na watoto....nyie mnatoka Weekend sie twatoka J'tatu....kisa na sababu? Ili tusiwe sawa, hakuna lingine wacha kutuJAJI eeh! Nasikia Asali wa Moyo analalamika "mijaume ya kiafrika sijui ikoje (yeye mwenye Muafrika) inamkodolea macho mke wa mtu wakati inaona kabisa yupo na Mtu wake" Hee! Nka