Skip to main content

Posts

Akina sie on Budget...

Ili kuifanya itoke vizuri huwa tunajiita "the simple life" women....well U-simple unatofautiana nadhani unalijua hilo. Mfano hapa hunikuti na hautonikuta nazungumzia Manunuzi ya Wiki au Mwezi huko High end (Designers) pamoja na hilo pia hunikuti nazungumzia Maduka ambayo ni Lowest End.....mie nipo kati. Napenda Ubora, Mfano Bag lazma iwe Real/Genuine Leather kwani ndio my Kitu sio Trends. Sasa si nilipita kwenye Charity Shop maeneo wanayoishi Mastaa Jumamosi iliyopita, nikakuta watu Kibao kwa nje....nkauliza kwani kuna Star humo ndani? Wakasema hapana ila kuna "new stock" by new wanamaanisha Stars wame-donate Ma-used-designer Gear jana yake. Aii! Mwanamke sijawahi kumiliki Designer Bag Genuine....wee! Mie huyu ninunue Hand Bag kwa £2,340 wakati hata Tofali la Choo (sio Jimmy Choo, Choo as in Toilet eeh) sina.....hata Fake ones sina. Nikaweka u-simple pembeni....nkaunga foleni....nkajipatia "Chloe Python Paraty Tot

Happy December.....nimekuwa huru!

Nikajikuta nashindwa kusoma maandishi au kutambua Sura ya mtu kwenye Tv au popote pale ambapo ni umbali wa hatua 4, sasa naona (Navaa Miwaani baada ya kuikwepa kwa Miaka zaidi ya 15). Halafu Binti kaacha kunyonya full-time (haombi na wala hadai) hooray...whoop!...whoop! Sasa siku moja nipo Bafuni najilola(najiangalia) nikaona pale nyuma kati pamekuwa a bit "firm" and more Duara(maana ukizaa matako yanashuka/tepeta kidogo ujue)....nkasema wohooo mazoezi yangu yanalipa! Kuja kuhamaki....kumbe nimenenepa hihihihihihi(nlijipima kitu kutoka 32inch to 46). Side effects za kuacha kunyonyesha nazo, mxsiii (kama unataka kuzijua zote nitafute nikumwagie mauzoefu). Na mwisho kabisa Asali wa Moyo anaumwa "Flu"(Homa, body ache, Kikohozi na Mafua).......si unajua wanaume wakiumwa "Flu"...full kudeka hehehehe I mean "hoi" imagine wangekuwa wanazaa the Puuzi kabisa! Babai. Mapendo tele kwako...

Wale "naenda Africa", Natoka Africa....

Unawajua? Huwa hawasemi Nchi zao.....mf: unauliza (kwa kizungu) unatoka wapi? Wanasema "Africa"....where about in Afrika...."East Africa"....yes...where exactly? Sasa tangu Ebola ime-"cotton fire" Afrika inaitwa the Land of Ebola....hihihihihi watu hawasemi tena wanatoka Afrika bali Tanzania au nchi yeyote ambayo sio Magharibi ya Afrika (au karibu)! Kuna jamaa enzi akiwahi kusema (na wakamuamini) kuwa yeye anatoka Afrika, akaulizwa Afrika wapi....akasema "a small Country inside Tanzania called Tabata" na Baba yake ni King of Tabata! Mie siipendi Tanzania Kisiasa(sipendezwi na Siasa za Tanzania), lakini naipenda kama Nchi niliyozaliwa, na ndio maana sina (nimekataa) Ganda Jekundu kwa makusudi kabisa....(Kwa faida ya Wanangu)! Nilivyojihami hapo juu! Babai. Mapendo tele kwako...

Vyombo vya Wageni....!

Vinakaa Kwenye kabati KUUUUUUUbwa sebuleni (I used to hate that thing)....ila nilikuwa naelewa kwanini wengi wao (nilikuwa mtoto so simo) huwa na Kabati la vyombo (vitumiwavyo only wageni wakija) Sebuleni. Nyumba nyingi za kupanga ama Mna-share jiko au kila mtu anapika Sebuleni kwake kama sio nje ya mlango wake pale Koridoni/kwa nje, hivyo kuwa na Kabati la vyombo Sebuleni inaleta maana(Wapangaji sita, wote muweke makabati yenu jikoni? Hapatatosha). Achana na hilo...turudi kwenye "vyombo vya wageni"....mpaka leo (well mwaka juzi niliponunua Gold China Dinning Set and Tea Set*) ndio nimeelewa umuhimu wake. Kuwa sahihi naweza kusema nimejua umuhimu wa viatu vingi baada ya kuwa "Temp house wife", vitu kama vile kusafisha nyumba mara kadhaa kwa siku (nlikuwa nasafisha once a week, ile deep cleaning). Sasa nikienda madukani, lazima nikasalimie kwa akina "Home Departments"....yaani hadi nimeanza kuwaza mambo ya kuwa &