Baadhi ya watu hasa Vijana wanapenda sana kuonyesha "hisia" zao kwa vitendo, katika umri mdogo ambao ndio kwanza unajifunza Ujinsia wako, "Affection" goes a long way. Katika hali halisi huitaji zaidi ya kuhisi unapendwa na kupata uzoefu wa mwili wako unavyoibua Msisimko wa raha ambao hujawahi kuuhisi tangu Ubalehe/Vunje Ungo. Wengi huamini wapenzi wanaofanya hivyo basi huwa na uhusiano/ndoa yenye Afya. Ukweli ni kuwa sio mara zote, sio tu kwamba kuna wakati mnajikuta hamna muda kutokana na mtindo wa maisha ya sasa bali inapoteza uzito/umuhimu(ni vema kuirudisha time to time). Utajiuliza kwanini kuonyesha "hisia" zako kwa vitendo kuharibu uhusiano/ndoa wakati ukifanya hivyo unajisikia vizuri/raha na kuwa karibu zaidi na mwenza wako? Jibu ni rahisi tu, Kwenye Ndoa kuonyesha Hisia zako ni rahisi kuliko kukabiliana na "issues" kubwa au hata kuchangia maoni yako au kumshauri mwenza wako labda kikazi, kifamilia(kule alikozaliwa), maendeleo n