Skip to main content

Posts

Saikolojia ni Sayansi rahisi, you need to heal...

...huwa wanamaanisha nini? ku-heal ndio kukoje wakati huna matatizo ya kiafya(kimwili)?  Kuna maneno watu wa mitandaoni wanapenda kuyatumia ili kuonekana wajuzi au wana upeo ama wana akili/wasomi(kila mtu anataka kuonekana hivyo), unakuta mtu anajieleeeeeza halafu hakuna anachoelezea, anajazia tu maneno ambayo yana-sound vizuri au kisomi ama yale "clinical" yanayotumiwa zaidi ya Wanasaikolojia(wale wenye Leseni ya kutoa Huduma hiyo baada ya kumaliza masomo na kufuzu kwa kiwango cha phD) au Madaktari wa Akili Sisi tuliosoma "Social Science" kama sehemu ya Kozi nyingine hatupaswi ku-act kama vile ni Wanasaikolojia, ni kama Sheria kuna sehemu unaijua na unaweza kuizungumzia lakini wewe sio mwanasheria, uliisoma tu kama sehemu ya Kozi yako na sio Kuisomea. Huezi amini leo ndio nimeelewa kwanini Wanasheria wa Bongo huitana "Mwanasheria Msomi". Juzi hapa nilikuwa nasikiliza PodCast(yeah them ones) kuhusu malezi ya watoto kutoka kwa "wataalamu", kukawa

Tangu umefunga ndoa, ume-improve...

 ..Mchezo au upo vile vile? Kwamba ya nini ni-showcase  au ujiboreshe wakati  umeshampata, ni wako mpaka kifo? Sio sasa ni wangu wacha ni practise nae zaidi na time to time ni showcase niliyofuzu? nayo hapana? Ndoa ikibuma je utaanza kujifunza upya?  hehehehe hawa wa siku hizi hawajui kusubiri, yaani hata muda wa ku-show off maujuzi hupewi.....ukitoka na hujalipia  meal, umeachwa(wakati haukuwa na uhusiano nae)....hii kwa wote, wewe na mkeo/mmeo.  Natambua kuna kubadilika au tuseme kukua(inategemea na umri mliofunga ndoa)....uboreshaji  wa tabia au mtindo wa maisha ni jambo muhimu, maana huwezi kuishi kama kijana/binti wa miaka 32 wakati sasa una miaka 47...Wataalamu wanasema kuwa Uhusiano haubadiliki bali wenza ndio hubadilika, mimi nabisha kwasababu ninyi mkibadilika/kua ni wazi kuwa mahitaji yenu yanabadilika na hivyo uhusiano mzima kubadilika.  Mfano; Uhusiano wenu ulivyokuwa kabla ya kufunga ndoa ni tofauti na sasa mmefunga ndoa, na uhusiano huu baada ya ndoa hubadilika baada ya k

Imani ya Dini ni Msingi mzuri kulea watoto....

  Pamoja na kusema hivyo haina maana kuwa Dini ndio kimbilio kwasababu ukizidisha huko Dinini pia unaweza kuongeza viungo kwenye matatizo yako ya akili au kuongezea mengine. Unapokuwa unafuata Imani ya Dini (Traditional Churches na Uislamu, hao matawi ya ukristo wa kisasa aka MATAPELI mie siwatambui) inakusaidia kuishi kwa heshima na kufuata princimples zake, unajua nini chakufanya(unamkimbilia Mungu) unapopata matatizo   mfano kupoteza kazi, migogoro kwenye urafiki, wazazi, ndoa, ndugu au hata pale unapoyumba kiimani.   Sio tu kwamba unakuwa na kimbilio (Mungu) bali pia unakuwa na Community kutokana na Asilia yako(Kabila) ambayo kwa kiasi kikubwa mnakuwa mnajadili masuala mbali mbali ya kimaisha na mnakuwa na activities hata kama ni mara moja kwa Mwaka, mnakuwa karibu kwavile mnamisingi inayofanana, mnaiheshimu na hivyo inakuwa rahisi kuepuka “Drama” ambazo ni chachu ya matatizo ya Akili.     Kutokana na muibuko wa social media, kumekuwa na watu wakipeana mioyo au kufundishana

Jinsi ya kurudisha Furaha Ndoani 2...

  Yafuatayo yatakusaidia kurudisha furaha kwenye Ndoa yenu ikiwa mtashirikiana na kuyafanyia kazi. Yote haya mmeishawahi kuyaishi hivyo hakuna ugumu/jipya, sema tu mmezeoana so mnayachukulia kawaida, kwamba hayana "maana/umuhimu" kwa sasa.   -Wote; Acha yaliyopita huko huko yalikopita, kamwe usiayarudishe tena kwasabau tu unataka kushinda mabishano au unataka kumkumbusha mwenzio ni kiasi gani umemsamehe au namna gani alikuwa bwege hapo zamani za kale ili kumshusha na kumuumiza hisia zake(huo ni utoto).   -Wote; Unakumbuka enzi zile kabla hamjawa wazazi? Mlikuwa lovers, natambua hii inaweza kuwa ngumu hasa kwa sisi wanawake(wake)kwasababu katika haki halisi tumebadilika kiakili, kimwili na kiafya. Uzazi ni kujitolea mhanga, uzazi unakuja na trauma sio kimwili tu bali kiakili, Uzazi unabadilisha namna unamuona mumeo sio kwamba anapoteza umuhimu bali unahisi hakuhitaji tena kwasababu kuna kichanga.   Waume zetu mpo vile vile kimwili kwasababu hamkubeba mimba na hamk