Skip to main content

Posts

Enzi tulitongozwa uchochoroni...

Miaka 10 iliyopita mlitongozana kwa texts au kwa sauti baada ya kuona picha, nasikia siku hizi wala hamtongozwi kabisa au nyie ndio mmekuwa watongozaji. Wanawake wamekua wawindaji, watafutaji, wapiganaji....wanaume wanafanya nini?  Basi sie "Mid Gen X" a.k.a Xennials a.k.a MillenX (tulizaliwa 1975-85) tulikuwa tunakimbiliwa huku tunaitwa " oyaa mrembo" au "oyaa dada'ke (weka jina la kaka yako)" au hey Binti (weka jina la Baba yako), kama jamaa humtaki/hakuvutii unakimbia kama athletes au unaingia kwenye nyumba yeyote unatulia mpaka jamaa apitilize au ageuze na kurudi kijiweni, then unaendelea na safari zako au inatokea mtu kwenye nyumba hiyo anakisindikiza so unakuwa pretected. Kama jamaa unamkubali basi unapunguza mwendo so anakufikia haraka.  Mnatembea huku anakuuliza maswali kisha mnafika kichochoroni(hakuna watu wengi) then anashusha mistari yake...unadengua-dengua pale na kujiringisha(hiba ya kike) huku unachora chini au unatafuna kucha...unamuang

Asking for money, mmepoteza aibu online?

Majuzi nilikuwa nakatiza mitaa ya YouTube  nikitafuta best  Female TV talk show Bongo Tanzania baada ya kukumbuka enzi nikiwa msichana kulikuwa na kipichi cha wanawake, siku mbuki jina wala Host wake ila Jaquline Ntuyabaliwe (sasa Mrs Mengi) alikuwa mshiriki, ilidumu kama episodes 3 hivi(kila Ijumaa/Jumamosi)..unfortunately sikupata nilichokuwa natafuta ila  nikakutana na podcast/Youtube Channel ya Salama, nikawa nasikiliza mazungumzo na mgeni wake, which was quite interesting then kwa chini I saw there were kijibango anaomba "kuchangiwa" as in donate to the channel/podcast, I thought these people have no mshipa wa aibu.  Am used to other youtubers asking for money or as they demand "cash Up me:, "donate first ndio nitaanza kuongea", "join my channel  for elfu 3(£1) kwa mwezi to get exclusive"...but Dada si Muajiliwa kule Sekta ya private which they pay better than Serikalini...No? au mazungumzo yake na Mastar ni side haso?  Huwa najiuliza, I (you) su

Endelea mtongoza Wife...

Ni kawaida kwako Mume (na jamii kwa ujumla) kutegemea mkeo afanye kila awezalo kuifanya ndoa kusimama utasema kajioa mwenyewe. Kuna siku nikaamua kugugo matatizo ya Ndoani, kila maelezo niliyoyapata kwa Kiswahili na Kiingereza, mzigo wa kuweka mambo sawa wenye Muungano huo alibebeshwa mke.   Hakukua na maelezo ya kutosha ambayo yanamsaidia Mume kutatatua matatizo ya ndoa zaidi ya nini afanye akishindwa kusimamisha, Mke na Mama nani nimpende? au nini cha kufanya ikiwa anamaliza haraka? Vipi kuhusu nini cha kufanya ikiwa umemuudhi mkeo? Nini mbadala wa kumnunia/fokea/ignore mke wangu, kitu gani nifanye kukabiliana na mzunguuko wa hedhi wa mke wangu baada ya kupevusha pale anapokaribia Siku zake(sio za kufa bali Hedhi) n.k.? Kuna mengi kwenye ndoa zaidi ya Ego, Mama yako na Uume wako.     Kwenye blog hii tutakumbushana mengi tu ambayo hayahitaji uekisipati wa jinsia bali ni uelewa wa kawaida tu wa kusomana kwa pande zote mbili. Nakumbuka enzi nilipokuwa Twitter kuna wakaka wawili nawahesh

Saikolojia ni Sayansi rahisi, you need to heal...

...huwa wanamaanisha nini? ku-heal ndio kukoje wakati huna matatizo ya kiafya(kimwili)?  Kuna maneno watu wa mitandaoni wanapenda kuyatumia ili kuonekana wajuzi au wana upeo ama wana akili/wasomi(kila mtu anataka kuonekana hivyo), unakuta mtu anajieleeeeeza halafu hakuna anachoelezea, anajazia tu maneno ambayo yana-sound vizuri au kisomi ama yale "clinical" yanayotumiwa zaidi ya Wanasaikolojia(wale wenye Leseni ya kutoa Huduma hiyo baada ya kumaliza masomo na kufuzu kwa kiwango cha phD) au Madaktari wa Akili Sisi tuliosoma "Social Science" kama sehemu ya Kozi nyingine hatupaswi ku-act kama vile ni Wanasaikolojia, ni kama Sheria kuna sehemu unaijua na unaweza kuizungumzia lakini wewe sio mwanasheria, uliisoma tu kama sehemu ya Kozi yako na sio Kuisomea. Huezi amini leo ndio nimeelewa kwanini Wanasheria wa Bongo huitana "Mwanasheria Msomi". Juzi hapa nilikuwa nasikiliza PodCast(yeah them ones) kuhusu malezi ya watoto kutoka kwa "wataalamu", kukawa