Skip to main content

Posts

Showing posts from January, 2015

Bichwa kubwaaa tiny brain......

Women....sio kwamba tuna mabig head bana ni nywele tu hizo. ...Pia hatuna tiny Ubongo isipokuwa sehemu kubwa ya Ubongo wetu inatumika. Yaani tunatunza mambo mengi sana na hufanya tuwe na kumbukumbu nzuri kuliko wenzetu.... si wajua Data zikikaribia kujaa kwenye PC au Simu which is PC. ...isn't it?.....speed inapungua. Unajikuta unakuwa mvivu kufikiria kwa undani kabla hujasema matokeo yake unatoa lolote halafu unagundua neno likitoka halirudishiki.....unabaki kujuta au ku justify. Wanaume ambao walikaribia wanawake ni wale waliotumia 1/3 ya Ubongo wao na baadhi yao ni JK Nyerere, Gandhi na B Mkapa(no Nkapa really I just liked him as prezzo). Kama hutaki kuamini nikuambiacho kuhusu matumizi yetu ya Ubongo nenda kaGUGE. (Googling......kaguge usisahsu you heard it here 1st). Binafsi huwa nafikiria huku naongea au kuandika na matokeo yake huwa si justfy bali nasimamia nilichokisema na kukusaidia kunielewa. So wacha uvivu, soma magazeti ambayo ni broadsheet sio tabloids. ...wacha bl

Kukazika Kazini na Kukazika nyumbani....

Wapi kuna nafuu? Najua utasema nyumbani kwasababu unajipangia nini cha kufanya wakati gani......wakati Kazini haipo hivyo,  unafanya jnachotakiwa kuganya kwa wakati husika. Pamoja na kuwa unajipangia kazi zako ukiwa nyumbani bado kazi hizo zinachosha zaidi hasa ukiwa na watu to kuliko yule ana kwenda Kazini nje ya nyumbani. Unafuu wa kukazika nyumbani hutoweka kabisa kwasababu hakuna kutoka nje ya mahali pako pa  kazi na kamwe hakuna Likizo. Angalia anaekazika Kazini nje ya nyumbani ana mahali pa kwenda ambako ni nyumbani......na ukifikika huko unapokelewa kwa furaha na watoto wenye afya njema, unakuta nyumba safi, chakula kimeandaliwa na mengi neyo. Ukipiga kazi I mean ukikazika vya kutosha unachukua day off au likizo kabisa kutoka mahali pako pa kazi na kwenda kupumzika nyumbani ambako ni mahali pa kazi kwa mwenzio asiekujua na day off walaaa Likizo. Daah mlango si umegongwa, kufungua nakutana na jirani kaja jitambuliaha as ndio kahamia mtaani.....hayo ma hug niliyopewa s

Mtu wa ku-share nae matatizo yako!

Ni nani? Kuna wakati unahisi kupata mtu wa kumuambia matatizo yako ili kushusha mzigo wa mawazo.......Kama ujuavyo kulizungumzia tatizo kunakusaidia Kisaikolojia kuhisi uzito wake mabegani umepungua. Mara zote huwa tunakimbilia kwa wazazi, ndugu, jamaa na marafiki. .....mara chache huenda kwa Viongozi wa Dini. Mzazi huwa anakusikiliza na kukupa matumaini,  ndugu na jamaa hutoa ushauri pia marafiki hujitahidi kutoka mawazo yao. Mzazi kamwe hawezi kusambaza habari za tatizo lako kwa mtu mwingine hata kama ni dada yako mpaka labda aone kuwa maisha yako yapo hatarini. Ndugu....er inategemea maana kuzaliwa baba moja na mama mmoja sio lazima mpendane....marafiki nao hupeda kufananisha matatizo ya mtu na mtu na bila kujua wanajikuta wame-share matatizo ya wenzao na wengine ni wazuri kusikiliza na kushauri kisha wanakucheka au unakuwa hadithi ya kushangaza au kuaikitisha kwao. Viongozi wa Dini wa kisasa hutumia info za matatizo yako kama mfano au shuhuda kwa Waumini wao. Wengine hutumia

Men are Stronger than Women...

Kweli kabisa.... Wanaume ni Imara na wenye Nguvu "kimwili" (Misuli) kuliko sisi Wanawake lakini ukweli ni kwamba wengi wao ni "wadhaifu" sana kwa ndani (emotionally). Hukimbia matatizo au Changamoto za kifamilia badala ya kukabiliana nazo kwa ushirikiano na wake zao. Wapo radhi kuanza upya kuliko kukabiliana na changamoto za "life situations" mf, Magonjwa, Vifo, Ulemavu, ukosefu wa Kipato(pesa) na mengine yote ambayo sio "choice". Mwanamke humvumilia mwanaume kwa yote hayo niliyoyataja hapo juu na mengine ambayo ni "life choice" (hayavumiliki) ya Mume mtu....mf Ulevi, parting, Ufuska, Ubahili n.k. Uimara wetu ki-emotonal na ile motherly (sijui nini) tuliyoumbwa nayo hutufanya tubaki kwenye Ndoa/Uhusiano na kuwauguza wenzetu.....hali hii huwafanya baadhi yao kwenye Jamii kuamini kuwa ni "jukumu la mwanamke". Ukweli ni kuwa sio "jukumu" bali ni Umara wetu ka