Skip to main content

Men are Stronger than Women...

Kweli kabisa....


Wanaume ni Imara na wenye Nguvu "kimwili" (Misuli) kuliko sisi Wanawake lakini ukweli ni kwamba wengi wao ni "wadhaifu" sana kwa ndani (emotionally).





Hukimbia matatizo au Changamoto za kifamilia badala ya kukabiliana nazo kwa ushirikiano na wake zao.





Wapo radhi kuanza upya kuliko kukabiliana na changamoto za "life situations" mf, Magonjwa, Vifo, Ulemavu, ukosefu wa Kipato(pesa) na mengine yote ambayo sio "choice".





Mwanamke humvumilia mwanaume kwa yote hayo niliyoyataja hapo juu na mengine ambayo ni "life choice" (hayavumiliki) ya Mume mtu....mf Ulevi, parting, Ufuska, Ubahili n.k.





Uimara wetu ki-emotonal na ile motherly (sijui nini) tuliyoumbwa nayo hutufanya tubaki kwenye Ndoa/Uhusiano na kuwauguza wenzetu.....hali hii huwafanya baadhi yao kwenye Jamii kuamini kuwa ni "jukumu la mwanamke".






Ukweli ni kuwa sio "jukumu" bali ni Umara wetu kama wanawake.....japo ni wepesi kulia, wepesi kulalama na kuwa mood pale tunapohisi kuachiwa kufanya kila kitu (single mother with a husband), wepesi kushitaki lakini bado ni Imara sana kuliko Wanaume.





Sasa huku nliko, wanataka kufundisha wanaume namna ya kuwa Baba wazazi na sio "Baba uliechangia tumbegu" kwa Dakika 3 za Ngono....ili kuepuka uwingi wa "single" mothers na hivyo kuokoa Ndoa kwa faida ya watoto...er na ku-save money!




Dakika 3 (if you are luck that is) za ngono zinaeza mfanya mwanaume yeyote kuwa Baba.....Kuwa Baba mzazi unahitaji kutumia muda wako kumjua mwanao, kumsaidia(kuoga/vaa), kumfundisha(manners), kucheza nae n.k.




By the path kumnunulia mtoto zawadi ghali na kumwambia unampenda haitoshi kuwa "baba Mzazi".....step up!




Nimekukwaza baba? Just unread my Post hihihihihi.....Heri ya Mwaka Mpya!!


Babai.
Mapendo tele kwako...

Comments

Christian Bwaya said…
Huu mbona ni ukweli mtupu? Niliwahi kuandika kitu kinachofanana na hiki, kuonesha udhaifu wa mwanaume.

http://bwaya.blogspot.com/2014/10/kuogopwa-kwa-wanawake-wenye-mafanikio.html

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao