Monday, 16 July 2018

Muendelezo wa Twiti yangu ya "if he is hot, don't let yourself go"...


Miaka mitatu iliyopita niliandika kuhusu Wanaume wapenda nachuro byuti, kama ilikupta isome hapa kisha tuendelee. Kwanza habari za leo? mie nipo Likizo, aina ya Likizo ambapo unafanya yote uyafanyayo unapokuwa nyumbani isipokuwa haupo nyumbani. Achana na hili.


Kuwa shabiki wa "natural beauty" wakati unavaa Nguo, unaoga maji Safi ya Bomba(yana Kemikali), unavuta hewa kila siku(imejaa toxic), unakula vyakula vinavyotunzwa kwa kutumia Kemikali ili kuepusha magonjwa/wadudu, Ukiugua unatumia Tiba ya Kisasa, Unatumia Simu kuwasiliana  n.k. sio rahisi.Hakuna tatizo la mtu kupenda Urembo wa Asili na hakuna tatizo kwa yeyote anaependa Urembo wa kununua/jiongezea ailimradi tu hambadilishi na kukufanya uonekane mtu mwingine. Imekuwa ni kawaida kwa baadhi ya wanaume kusakama Wanawake wanaopenda kujiremba(usually wasio kuwa na pesa, maana makeups sio chee).


Kutokana na maisha yalivyo  hivi sasa (Wanawake tunafanya yaliyokuwa yakifanywa na Wanaume pekee) na mabadiliko ya Hali Nchi(are those words?) inakuwa  ngumu kwa Mwanamke kuonyesha "unamake wake" na hivyo wengi kujikuta wanakuwa kama Wanaume kima vazi, kimaongezi na wengine mpaka miondoko inabadilika hihihihi ili tu "kuheshimika" aka wasionekane wanavutia.
(Unajisemea ge to to the point Dinah hehehe nakusikia)


Wanawake tunapenda kuonyesha uanamke wetu kwa aina mbali mbali tofauti, nyingi huwa faraghani/nyumbani na chache kwenye kadamnasi mf, jinsi tunavyotembea, mavazi, kujiremba/pamba/jipenda,  jinsi tunavyo ongea, kula n.k.


Uanamke wetu huyumba tunapojifungua au tunapokuwa na Mwanaume ambae anadai kuwa anapenda nachuro byuti yako  huku yeye anajipendezesha na daily yupo "Hot" kimuonekano. na wewe unaonekana kama msaidizi wake na sio mwenza wake. lakini unajiachia tu na huoni sababu ya kujijali/penda/remba kwa sababu Mumeo anapenda Unachuro wako.


Mumeo ambae Hot sio anajipenda for nothing, huko endako anakutana na "hot" wenzie, anaona wanavyopata attention na pengine na yeye anazitoa na kuzipokea lakini hataki kabisa wewe uzipate na hivyo kumpa amani Moyoni kuwa Hakuna "hota" mwingine atakaevutiwa na wewe kwasababu sio "hot". Ana uhakika kabisa wewe huwezi kuvutiwa na "no so hot" kwasababu yeye ni "Hotter"...sijui umenielewa?


Kama mumeo anajipenda(ata asipojipenda) hakikisha unajipenda, unajijali....nyumba haihitaji wanaume wawili bali Mwanaume na Mwanamke, tumia uanamke wako kuweka tofauti hiyo wazi. Jirembe, Fanya  mazoezi(kwa afya sio kukonda), remba nyumba yako, usafi wa mazingira(sukuma mumeo na watoto wasaidie).

Marehemu Bibi yangu (mfundaji) alinambia "Ukiolewa sio ruhusa kwa wanaume wengine kuona Sura yako ikiwa Uchi, hiyo sura ni kwa ajili ya Mumeo tu hivyo jirembe"....mimi nakuambia ikiwa mumeo anavutia, mtanashati usijiachie Jirembe, pendeza,vutia.

Tambua nathamini Muda wako hapa, ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Bai.

Sunday, 15 July 2018

Kuwa "affectionate" kwa Mwenza wako kunaweza haribu Ndoa/Uhusiano wenu...Baadhi ya watu hasa Vijana wanapenda sana kuonyesha "hisia" zao kwa vitendo, katika umri mdogo ambao ndio kwanza unajifunza Ujinsia wako, "Affection" goes a long way. Katika hali halisi huitaji zaidi ya kuhisi unapendwa na  kupata uzoefu wa mwili wako unavyoibua Msisimko wa raha ambao hujawahi kuuhisi tangu Ubalehe/Vunje Ungo.


Wengi huamini wapenzi wanaofanya hivyo basi huwa na uhusiano/ndoa yenye Afya. Ukweli ni kuwa sio mara zote, sio tu kwamba kuna wakati mnajikuta hamna muda kutokana na mtindo wa maisha ya sasa bali inapoteza uzito/umuhimu(ni vema kuirudisha time to time).Utajiuliza kwanini kuonyesha "hisia" zako kwa vitendo kuharibu uhusiano/ndoa wakati ukifanya hivyo unajisikia vizuri/raha na kuwa karibu zaidi na mwenza wako? Jibu ni rahisi tu, Kwenye Ndoa kuonyesha Hisia zako ni rahisi kuliko kukabiliana na "issues" kubwa au hata  kuchangia maoni yako au kumshauri mwenza wako labda kikazi, kifamilia(kule alikozaliwa), maendeleo n.k.Pamoja na kuwa "affectionate" ni muhimu, kumbuka sio muhimu kila wakati kila siku, wakati mwingine Mume/Mke anahitaji zaidi kutoka kichwani kwako(Matumizi ya Akili) na sio kushikwa-shikwa(tomaswa), lambwa-lambwa(mabusu), nuswa-nuswa au kukumbatiwa na kunong'onezwa.


Stori time: Nimewahi kufanya kazi(ya kushauri) Pea moja kitambo hivi, Mke mtu alikuwa mzuri kweli kwenye kuonyesha "hisia" zake  kwa vitendo kwa mumewe wa Miaka 12. Lakini akawa anashangaa kwanini  siku hizi Mume wake haonyeshi furaha kama awali. Akawa anahisi labda mumewe kapata mtu mwingine nje ya Ndoa yao.


Mume mtu alikili kuwa anashukuru kuwa anaporudi kutoka Kazini Mkewe anampokea kwa furaha, kumkumbatia na kumpa mabusu kendekende, wakati mwingine kumuandalia "bath" maalum na kumkanda mwili ili kuondoa Uchovu. Lakini pamoja na yote hayo bado anahisi anahitaji zaidi kutoka kwa Mkewe, kwamba anahitaji Ushauri/changamoto na kuwekwa sawa zaidi ya kusikilizwa na kupozwa kwa "affection".


Natambua kuwa Wanawake wengi ambao ni "traditional" lakini tumetoa mavumbi machoni(mimi Mmoja wao) tunapenda kuwafanya waume wetu wajione "Wanaume" kwa kuonyesha nguvu yetu ya u-feminin. Tatizo baadhi hupitiliza au hawajui namna ya ku-balance the two. Kwamba kuwa wa Kizamani na wa Kisasa kwa wakati mmoja.


Ni muhimu kwenda na wakati lakini usisahau Asili ya Mwanadamu, Mwanaume anapenda kujiona/hisi  kuwa Uanaume wake unaheshimiwa na Mwanamke anapenda kuhisi Uanamke wake unathaminiwa. Lakini hapo hapo Ndoa/Uhusiano wa "ndio bwana" na too much affectionate hupelekea upande mmoja kuhisi haupati Changamoto na hivyo kwenda kuisaka kwingine au kuwa mkorofi(jinsi anavyo ongea na wewe) ili tu Usimame na kumuweka sawa.Changamoto ninayoizungumzia hapa sio ya kuongeza Kimada, kama ambavyo baadhi ya wanaume Tanzania wanavyo amini kuwa ili Mkeo "achangamke" basi mtafutie mwenzie....hilo sio suluhisho bali unyanyasaji wa Kihisia, Kisaikolojia na Kakili kwa Mkeo na watoto wenu,


Changamoto ninayozungumzia hapa ni Mf: Mume kaleta  wazo la Mradi mpya na anakuelezea jinsi gani ataufanya n.k., wewe unaishia kumpongeza na kutoa maafeksheni yako, badala ya kuhoji na kutoa maoni yako kulingana na maelezo alioyokupa ili kumuongezea "ideas".


Au amekuwa akifanya Shughuli ile ile tangu mmekutana na haionyeshi kuboresha maisha yenu, badala ya kumpa changamoto  na kumsaidia/fanya awe "ambitious" wewe unaendelea tu kutoa mafeksheni yako na "ndio bwana" zako na kuishi kwa mazoea.


Wanaume hawafanani, kwasababu uliambiwa kwenu sijui kwenye Kitchen party au Imani yako ya Dini kuwa Mume habishiwi, mwanamke ni kukaa kimya haina maana Mume wako ni mmoja wa wale walio waoa hao watoa mafunzo.

Pamoja na yote, kumbuka Wanaume wengi wanapenda Changamoto.

Ahsante kwa kuchagua Blog hii. Nathamini muda wako hapa, mpaka wakti mwingine tena,


Bai.