Skip to main content

Posts

Showing posts with the label kujiamini

Kujiamini kwa Mtoto kunaanza lini?

....Watoto wa "Ulaya" wanajiamini sana, je kuna namna ya kulea mtoto ili akikua ajiamini kama wa Ulaya? Mkaka mmoja aliniuliza. Nadhani wengi wetu tumeaminishwa Mengi ya Ughaibuni ni Mazuri/Mema....lakini katika hali halisi sivyo. Kuna soko zuri sana la Vitabu/Vipindi vya TV vinavyofunza Wazazi namna ya kulea watoto wenye Kujiamini. Ni tatizo la Wazazi husika ambao walilelewa "Kimaendeleo" na hivyo kuhofia kuwa watoto wao watakuwa kama wao. Hofu hiyo inawafanya wazazi kuwa-overprotect watoto. Nahisi tu sina uhakika. Kujiamini kunategemea zaidi na Malezi(nakubali) lakini sehemu kuwa ya Mtu/Mtoto kujiamini inatokana na yeye mwenyewe alivyoumbwa. Niliwahi kugusia Bloguni hapa kuwa kuna baadhi tumezaliwa hivyo(tunajiamini) lakini pia wapo ambao hawajiamini mpaka wafunzwe/himizwa/pewa Moyo/saidiwa kujiamini. Naamini Watoto wa Afrika(well Tanzania wa kizazi kileeee) tunajiamini kwasababu tulitumia muda mwingi kujifunza kimwili na sio kihisia kama watoto

Jikubali, Jipende Jiamini so they say....

Habariiii! Baadhi huitaji support ili waweze kujikubali kujipenda na kujiamini halafu wengine tumezaliwa hivyo.....si vema kukurupuka na kumwambia mtu lazima ujiamini bwana blablabla.....sio chee kama udhaniavyo. Ni rahisi kujipenda, kujikubali na kujiamini angalau ukiwa umefikisha miaka 25(in my head umri huo ndio unaanza kujitambua na kujijua....unakuwa umekua). Mara zote Binti unapenda kuchukia baadhi ya vitu kwenye mwili wako hasa kipindi cha Kubalehe(tunabadilika). Huwa ni ngumu sana kukabiliana na mabadiliko ya ndani na nje ya mwili.....kiakili na kihisia. Kipindi hiki unaanza kujiona MZURI leo basi linapokuja suala la kuagizwa Dukani wewe ni wa kwanza kutaka kwenda ili "wakuone" si wajua kale ka atensheni ka wavulana kanakokusaidia kujua ujinsia wako? Kanakuwaga enjoyable sana......halafu kesho unakuwa MBAYA unagoma hata kwenda Shule unasingizia unaumwa er Macho (that was me). Ukifikia miaka 25 mabadiliko yanakuwa yameseto na kilichobaki ni kunenepa au kukonda. Un