....when Viongozi wote ni umri wako au wadogo kwako, Unakumbuka May 2, 1997 Tony Blair alikuwa Waziri Mkuu mdogo UK? Alikuwa kundi moja kiumri na Mama yangu ila sawa na Dingi. Hapa nilipo najihisi kama mama alivyojihisi mwaka huo(well I was not her then so I don't really know how she felt). Awali, binafsi nilihisi nipo nyuma ki-career kwasababu nilichukua time off kulea wanangu badala ya kuachia Childcare industry, sio hivyo tu kufanya kazi halafu mshahara wote unaishia kwa Walezi wa watoto wako ni dhambi. Yaani unabaki masikini halafu wakati huohuo huwajui wanao na wao hawakutambui kwasababu hujawahi kuwalea. Mbaya zaidi wakikua wanakuchukia na kumpenda Miss Amanda, kumsikiliza Mr Cook and kumuheshimu Mrs Mcmun huku wewe ukishangaa na kujiuliza kwani nimekosea wapi? Kwanini tabia haziendani na Values zenu(baba na mama). Mara pap! Nikakumbuka, Wakati wenzangu akina Macron, Jacinda wa NZ (alikuwa mdogo zaidi ila kazi ilimshida), Sanna Marin wa Ufini, Georgi...