Skip to main content

Posts

Siri ku-bounce back baada ya Kuzaa...

Mambo? Aah mie pia nimekukumbuka ndio maana nimeamua ku-blog kila siku kwa siku 5* kama zawadi yako ya  Christmas. Tegemea michapio kadhaa, nita-edit baada ya Xmas.   Now that is out of the way....njoo kwenye Somo la leo ila kama umekuja kujua namna ya kurudia mwili wako baada ya kuzaa, Pole ila usiondoke nataka nikupe siri yake ili ukome kutaka ku-bounce back haraka haraka, sio tu kwamba ni Kacha ya kimagharibi bali pia ni aina ya unyanyasaji wa jinsia kutoka kwa Mumeo. Maisha yangu yote nilikuwa chikonda aka skinny hivyo nilijizoea hivyo na nilijipenda nilivyokuwa. Baada ya kushika Mimba kwa mara ya kwanza nilinenepa na nilipojifungua mwili ukarudia wembamba wake ila nikawa  "shapely", kwamba nikawa na umbile la kike(vitu vikajitenga, nikatokelezea)zaidi. Hiyo ilichukua wiki 2, Mimba ya pili nikanenepa tena na mwili ukarudi ulipokuwa ndani ya miezi 2...baada ya hapo mambo mengi yakatokea kwenye huu mwili(story ndefu na sina muda) then akaja mtoto mwingine, tufanye ...

You know you are the oldest...

....when Viongozi wote ni umri wako au wadogo kwako, Unakumbuka May 2, 1997 Tony Blair alikuwa Waziri Mkuu mdogo  UK? Alikuwa kundi moja kiumri na Mama yangu ila sawa na Dingi. Hapa nilipo najihisi kama mama alivyojihisi mwaka huo(well I was not her then so I don't really know how she felt).   Awali, binafsi nilihisi nipo nyuma ki-career kwasababu nilichukua time off kulea wanangu badala ya kuachia Childcare industry, sio hivyo tu kufanya kazi halafu mshahara wote unaishia kwa Walezi wa watoto wako ni dhambi. Yaani unabaki masikini halafu wakati huohuo huwajui wanao na wao hawakutambui kwasababu hujawahi kuwalea. Mbaya zaidi wakikua wanakuchukia na kumpenda Miss Amanda, kumsikiliza Mr Cook and  kumuheshimu Mrs Mcmun huku wewe ukishangaa na kujiuliza kwani nimekosea wapi? Kwanini tabia  haziendani na Values zenu(baba na mama).  Mara pap! Nikakumbuka, Wakati wenzangu akina Macron, Jacinda wa NZ (alikuwa mdogo zaidi ila kazi ilimshida), Sanna Marin wa Ufini, Georgi...

Diaspora Wives...

...the long suffering ones wa US, UK and Canada nyie wa Scandinavia, Spain, Italy, Germany, etc hamuolewagi...wait, huwa hamuolewi na Waafrika wenzenu na wengi ni Mama wa nyumbani (natania). Dayaspora wives work several  shifts in the cold and spend the  money to support their husband's  business ventures in Africa. Them ones who want something back home, they want to become somebody somewhere kule kwa Motherland.  Mnakubaliana vema tu kuwa mara 4 kwa mwaka yeye atakuwa anaenda Tanzania au Kenya(depends on their origin) na kukaa huko kwa wiki 2 mpaka mwezi "kusimamia" Mradi/Biashara,  hiyo ni kila baada ya miezi 3.                                       picha kutoka gazeti la The Telegraph*? Kwasababu ya yeye kurudi kwao/kwenu mara kwa mara ni wazi kuwa haingizi kipato cha kutosha na hivyo yeye sio breadwinner isipokuwa wewe mkewe. Unajitolea mhanga ukiamini...

Enzi tulitongozwa uchochoroni...

Miaka 10 iliyopita mlitongozana kwa texts au kwa sauti baada ya kuona picha, nasikia siku hizi wala hamtongozwi kabisa au nyie ndio mmekuwa watongozaji. Wanawake wamekua wawindaji, watafutaji, wapiganaji....wanaume wanafanya nini?  Basi sie "Mid Gen X" a.k.a Xennials a.k.a MillenX (tulizaliwa 1975-85) tulikuwa tunakimbiliwa huku tunaitwa " oyaa mrembo" au "oyaa dada'ke (weka jina la kaka yako)" au hey Binti (weka jina la Baba yako), kama jamaa humtaki/hakuvutii unakimbia kama athletes au unaingia kwenye nyumba yeyote unatulia mpaka jamaa apitilize au ageuze na kurudi kijiweni, then unaendelea na safari zako au inatokea mtu kwenye nyumba hiyo anakisindikiza so unakuwa pretected. Kama jamaa unamkubali basi unapunguza mwendo so anakufikia haraka.  Mnatembea huku anakuuliza maswali kisha mnafika kichochoroni(hakuna watu wengi) then anashusha mistari yake...unadengua-dengua pale na kujiringisha(hiba ya kike) huku unachora chini au unatafuna kucha...unamuang...