Mimi sijui!
Hihihihihihi huyooo unapenda kutafutiwa kisha wee unameza tu (copy and paste)!!
Mwanamke mwenye maisha kama yangu (not exactly ila kwa mbaaaali) unawezaje ku-keep up na Blog updates kila siku?
Sio blog kama hii ambapo sihitaji kufikiri bali natiririka tu. Zile ambazo unatumia akili kimtindo kwa kuvuta kumbu-kumbu (Uzoefu) na kufikiri.......aiiiii Imenishinda!
Basi nimefika nyumbani siku hivi, nawakilisha nilichoambiwa na Walimu wa Babuu.....Baba mtu wacha aanze kung'aka....."Mimi sifuati wanachotaka wao kwenye nyumba zao za Kizungu, nafundisha mwanangu nijuavyo mimi".
Nikajiuliza kwa hasira bila kutoa sauti....hihihihi "sasa ni kwanini tunampeleka mtoto shule ikiwa hatutaki kuwa kitu kimoja na Walimu wake?".
Nikasema....Asali wa Moyo, shuleni kuna Mihula (mipya imeanza August) na ili watoto waimalize vizuri, kuelewa na kwa wakati ni lazima Wazazi wa-work together na Walimu, vinginevyo mtoto atakuwa