Skip to main content

Posts

Kwanini Mtoto awa wa Baba?!!

Nimekaa hapa nikafikiria(sio kweli)....limenijia tu kichwani. Kwanini tunaaminishwa kuwa Mtoto akizaliwa ni wababa, Jina lake la ukoo lazima liwe la Upande wa Baba. Ukimpa mtoto jina lingine la mwisho....baba anakuwa Mkali au anahoji kama kuna "mwenzie"! Kutokana na Mfumo Dume, nahisi(in my head) kuwa wali/na lazimisha hivyo kwasababu walijua/wanajua kuwa Baba ana sehemu ndogo sana kwenye Uumbwaji wa Mtoto. Baada ya zile Dakika Tatu (if you are lucky that is) kazi yake (baba) imeisha, isitoshe Mbegu hazina Damu so mtoto kuwa na Damu ya Baba yake ni kama 0.5% hihihihihi (lazma mnipige mkinikamata wababa). Hebu angalia suala hili kwa undani kwenye jamii bila kuhusisha Sayansi wala Dini! Kwanini hasa Babaz au ndugu Upande wa Mwanaume ndio huwa na viherehere vya kuendeleza Undugu kama sio kujishtukia kuwa hawana undugu (wanalazimisha). Stori time: Kuna siku nipo shereheni, mkaka mmoja akaanza kutambulisha ndugu wa Mama mbali-mbali l

"Ngoja nitakupigia" = Stop calling me....

Za milimo? Unawatambua wale watu ukiwapigia simu hawakawii kukuaga utafikiri wao ndio wamepiga....mnasalimiana vizuri, mara baada ya salamu...enhe nipe stori au "mamo mengine vipi?" Upande wa pili wa Simu(uliempigia) anaanzisha stori, unamsikiliza ukingonjea kwa hamu zamu yako ije ili uongezee kwenye stori husika (uongee).....yeye anakuambia " eh bwana eh, ngoja nitakupigia" halafu kimyaa. Baada ya Wiki kadhaa unampigia tena na kabla stori hazijachanganya yeye yulee "nitakupigia baada ya dk 20"....ndio imetoka hiyo mpaka umtafute tena. Mtu hutakiwi lakini hukomi mpaka mtu akuambie "sitaki Urafiki/Ujamaa/kujuana na wewe"....baadhi ya watu wanakupa "ujumbe" ili "muachane" vizuri bila kusutana, ukikimbiwa once na "nitakupigia baadae"....subiri mpaka akupigie (obviously hatokupigia). Unajua kuna watu wanapenda kuwa tegemezi kifikra.....hata sijui kama inaleta maana kwenye nili

Kutoboa Mtoto Masikio(Kutoga)

Ni umri gani hasa unapaswa kumtoga Binti yako Masikio? Na je yeye kutoga masikio na kuvaa Hereni ni muhimu kwake au kwako wewe Mzazi? Mie nilitogwa nikiwa mchanga (Miezi Sita) na nilichelewa, kutokana na Imani sijui Desturi ya mmoja wa Wazazi wangu ni lazima Binti wa kwanza atogwe na kuvalishwa Dhahabu. Binti yetu alipofikisha Miezi 3 Baba yake akasema tumpeleke akatobolewe(Togwa) Masikio, mie nikapinga na ku-suggest kuwa tumuache na akikua ataamua mwenyewe kutoga au kutokutoga. Nikaongeza, tena atakuwa na kitu cha ku-look forward to, mf: "nikifikisha miaka 15 natoboa Masikio".....kuliko tumalize kila kitu akiwa Mchanga halafu akikua tu tunaletewa Bf au Mjukuu kabisa sababu kila kitu tumekifanya akiwa bado mtoto. Isitoshe (in my head) tunatoboa watoto masikio kwa ajili yetu wenyewe Wazazi, yeye mtoto wala hajali kama anavaa Hereni ama hana "kitobo" cha kuweka Hereni. Baadhi ya Wazazi huku Ulayani wanachukulia kumtoga m

How to be Mum, Wife, HomeMaker and Blogger...

Mimi sijui! Hihihihihihi huyooo unapenda kutafutiwa kisha wee unameza tu (copy and paste)!! Mwanamke mwenye maisha kama yangu (not exactly ila kwa mbaaaali) unawezaje ku-keep up na Blog updates kila siku? Sio blog kama hii ambapo sihitaji kufikiri bali natiririka tu. Zile ambazo unatumia akili kimtindo kwa kuvuta kumbu-kumbu (Uzoefu) na kufikiri.......aiiiii Imenishinda! Basi nimefika nyumbani siku hivi, nawakilisha nilichoambiwa na Walimu wa Babuu.....Baba mtu wacha aanze kung'aka....."Mimi sifuati wanachotaka wao kwenye nyumba zao za Kizungu, nafundisha mwanangu nijuavyo mimi". Nikajiuliza kwa hasira bila kutoa sauti....hihihihi "sasa ni kwanini tunampeleka mtoto shule ikiwa hatutaki kuwa kitu kimoja na Walimu wake?". Nikasema....Asali wa Moyo, shuleni kuna Mihula (mipya imeanza August) na ili watoto waimalize vizuri, kuelewa na kwa wakati ni lazima Wazazi wa-work together na Walimu, vinginevyo mtoto atakuwa