Skip to main content

Posts

Vita ya Vibonge(plus size) kwenye Umodo!

Uchibonge aka Undimbo aka minyama uzembe....hello! Habari ya JumaSita? Jana nilikuwa naangalia kipindi cha Plus size War. Ambapo walizungumzia mengi kuhusiana na mwanamke kuwa mnene. Walianza na kuwasifia Bloggers wa Fashion ambao ni wanene halafu wakaenda ni nani hasa anapaswa kuwakilisha Plus sized women kwenye Umodo wa Mavazi to changamoto za wabunifu na waendesha maduka yanayouza nguo kubwa. Ila kilichonivutia zaidi ambacho nakiunga mkono kwa sababu nilikuwa najiuliza siku nyingi. Kwanini a size 14-16 anamodo kama Plus size? Well labda ni plus kwasababu UK size ndogo ya mtu mzima inayopatikana madukani ni 6 so ukiidabo au plus unapata 12 so year mie pia ni Plus size hihihihihihi. Mungu nisamehe. Binafsi nadhani Mawakala wa Plus size wanakosea.....japokiwa kwenye Documentary hii wamejielezea kwamba Soko walilonalo na demand wapatayo sio plus size tuitakayo watu wa kawaida kwamba ni size 20 to 34 au zaidi. Wanene hawana option linapokuja suala la fashion na Trend kwasababu mad

Elimisha mwanaume asibake(Rape) mwanamke....

....sio kufundisha Mwanamke jinsi ya kuzuia asibakwe! Habari ya wewe? Nasema ahsante kwa kuichagua Blog hii. Unategemea Nchi iliyoendelea kama UK kwamba huwezi kusikia suala la kuelimisha Wanaume kuhusu Ngono ili wasibake Wanawake via Media eti! Wapo wachache walioelimika na wenye kumthamini Mwanamke na kumheshimu na kutomjaji kutokana na Mavazi yake. Pia Hukumu kali dhidi ya Ubakaji inasaidia kwa mbali. Lakini bado kuna Wanawake na Wanaume ambao wanadhani kuwa Mwanamke kubakwa ni Kosa lake na hivyo kufundisha Wanawake namna ya kuzuia Kubakwa as in wasivae Mavazi yanayovutia Wanawame n.k. Mwanamke Habaki.....sasa kwanini yeye awe responsible kuji-limit kwa ajili ya Mwanaume? Kwanini Mwanaume asifunzwe kuji-control na kutomuona Mwanamke kama object ya kumalizia haja zake za Kimwili? Kanini Mwanaume asifunzwe kuwa ili kufurahia Tendo ni lazima au ni vema upande wa pili ukubali kutoa ushirikiano na sio kulazimishwa? Kwanini Mwanaume asionywe kuwa Kubaka ni Kosa? (Natambua wapo wan

Pale Gugo inapokuomba kutunza kila kitu chako...

Kuanzia Picha, Emails, Work Docs na bila kusahau details za kubanki Online. Habari ya J'pili na ahsante kwa kuichagua Blog hii. Kwa ubize wa maisha hakika utamshukuru Gugo kwa kukurahisishia......na yeye anakuukiza unataka nikumbuke pin au password yako fo yo konviniensi....na wewe unabonyeza Ok kwa hiyari kabisa. Tena inakuambia pia ni rahisi kufanya manunuzi online ukiseti Gugo loko(mahali ulipo)......na wewe unakenua na kukubali settings hehehehehe you are done Mwananchi. Baada ya miaka kupita utaanza kulalamika kwanini unaibiwa pesa au kwanini kila mtu anajua unapoishi. Ikitokea umefanya Jinai ndio utaijua Google na vitongoji vyake....siku itokee unautaka Ubunge sijui Uwaziri watu wanavuta Gugo na kupata kila kitu. Aiii nafurahia urahisi wa ku-shop online na kujua nini kinapatikana wapi lakini hayo mengine natunza na kukumbuka mwenyewe. Asante nashukuru Google. Well wanajua kila kitu cha yeyote anaewatumia isipokuwa hawawezi kuweka wazi details zako zipatikane kwa sabab