....sio kufundisha Mwanamke jinsi ya kuzuia asibakwe!
Habari ya wewe? Nasema ahsante kwa kuichagua Blog hii.
Unategemea Nchi iliyoendelea kama UK kwamba huwezi kusikia suala la kuelimisha Wanaume kuhusu Ngono ili wasibake Wanawake via Media eti!
Wapo wachache walioelimika na wenye kumthamini Mwanamke na kumheshimu na kutomjaji kutokana na Mavazi yake. Pia Hukumu kali dhidi ya Ubakaji inasaidia kwa mbali.
Lakini bado kuna Wanawake na Wanaume ambao wanadhani kuwa Mwanamke kubakwa ni Kosa lake na hivyo kufundisha Wanawake namna ya kuzuia Kubakwa as in wasivae Mavazi yanayovutia Wanawame n.k.
Mwanamke Habaki.....sasa kwanini yeye awe responsible kuji-limit kwa ajili ya Mwanaume?
Kwanini Mwanaume asifunzwe kuji-control na kutomuona Mwanamke kama object ya kumalizia haja zake za Kimwili?
Kanini Mwanaume asifunzwe kuwa ili kufurahia Tendo ni lazima au ni vema upande wa pili ukubali kutoa ushirikiano na sio kulazimishwa?
Kwanini Mwanaume asionywe kuwa Kubaka ni Kosa? (Natambua wapo wanaosingiziwa na wapo wanawake wanaobaka Watoto ni issue inayojitegemea siku ingine).
Kwanini kwenye kila Jambo baya linalomtokea Mwanamke kwenye Maisha yake hasa ya kimahusiano na Ngono ni kosa lake....(well isipokuwa Mimba, ni kosa lako sababu ni wewe ndio unaruhusu mtu akuwekee mananilihu yake).
Kwanini baadhi ya wanawake wanapend kuwatetea wanaume kwenye suala la Kubaka sababu ya aina fulani ya Mavazi ya Mwanamke?
Usilete suala la "sio Asili yetu....Utamaduni wetu" kwa wewe unaenisoma kutoka Pande za Afrika(Wasomaji wangu wanatoka Kenya...Burundi...Rwanda)....Mavazi ya aina zote sio Utamaduni wala Asili yetu.....tuliletewa kama tulivyoletewa Imani za Dini.
Sisi zetu zilikuwa ni Majani na Magome ya Miti....Vibwaya ambavyo vilikuwa vifupi.....na vijikamba ili kushikilia Jani la mbele lisianguke na kuonyesha Nyeti.
Mzungu(well na Mchina) huyo huyo ameamua kuboresha mavazi ya Asili yetu na sasa tunavalia "flori" sketi ambazo zimechanua na zina-move kama vibwaya.....nisizisahau Thongs ambazo ni kama vila walizovaa mabibi zetu miaka 9000 iliyopita (sina uhakika na namba hizo hihihihi but you get the idea).
Fundisheni Wanaume namna ya kuheshimu wanawake na chochote ambacho mwanamke anaamua kufanya juu ya Mwili wake....ni mwili wake hivyo anahaki na Mamlaka yakufanya chochote atakacho.
Mwanaume huna Mamlaka juu ya mwili wa Mwanamke.....unless ni mkeo in which nae pia atakuwa na Mamlaka juu ya mwili wako kama Mumewe.
Babai.
Comments