Uchibonge aka Undimbo aka minyama uzembe....hello! Habari ya JumaSita?
Jana nilikuwa naangalia kipindi cha Plus size War. Ambapo walizungumzia mengi kuhusiana na mwanamke kuwa mnene.
Walianza na kuwasifia Bloggers wa Fashion ambao ni wanene halafu wakaenda ni nani hasa anapaswa kuwakilisha Plus sized women kwenye Umodo wa Mavazi to changamoto za wabunifu na waendesha maduka yanayouza nguo kubwa.
Ila kilichonivutia zaidi ambacho nakiunga mkono kwa sababu nilikuwa najiuliza siku nyingi. Kwanini a size 14-16 anamodo kama Plus size?
Well labda ni plus kwasababu UK size ndogo ya mtu mzima inayopatikana madukani ni 6 so ukiidabo au plus unapata 12 so year mie pia ni Plus size hihihihihihi. Mungu nisamehe.
Binafsi nadhani Mawakala wa Plus size wanakosea.....japokiwa kwenye Documentary hii wamejielezea kwamba Soko walilonalo na demand wapatayo sio plus size tuitakayo watu wa kawaida kwamba ni size 20 to 34 au zaidi.
Wanene hawana option linapokuja suala la fashion na Trend kwasababu madukani wanatambua plus size ni kuanzia 14-18....kama ni size 20 au zaidi inakubidi uende kwenye Vibonge Speshalisti shopu.
Angalia hii ucheke au u uwe inspayadi.... https://youtu.be/My8jVUxvd7s
Halafu Gugo
Chanel4oD kisha tafuta Plus size War kama upo interested.....unaweza kipata idea ya Biashara kama ni smart enough.
Babai.
Comments