Skip to main content

Posts

Kula Fresh Vs Natural?

Hi.....kwa mara nyingine! Back in 2006 kulikuwa na mabishano kuhusu matumizi ya vitu ambavyo sio asili kwa matumizi ya Mwanadamu. Wengi wetu (tukisaidiwa na chunguzi mbalimbali) tuliamini kuwa matumizi ya vyakula vya Kopo, Madawa ya kutibu, aina za Sabuni, matumizi ya Microwaves n.k huenda ndio sababu ya magonjwa  Mengi yasiyotibika na kuu ni Saratani. Miaka ikapita na tukakugundua kuwa kutokana na Maendeleo ya Teknolojia kwenye kila kitu hakuna u-natural......kwamba hakuna mtu anakula kiasilia kwasababu mazao yote yanakuzwa na Mbolea ambayo ni "man made". Ukiachilia mbali Mbolea ni Maji tutumiayo kumwagilia mimea na madawa ya kuua wadudu wanaoshambulia Mazao.....Umepata idea ya wapi naelekea ambako sitaki kufika(sitaki post ndefu). Bado mabishano yapo au niseme yameamia kwenye utunzaji wa ngozi na Nywele. Watu wanajisifu kuwa wao ni Natural na hawataki Chemical(relaxer) kwenye miili yao lakini bado wanakunywa maji (bombani au chupani yote yanakemikali). Wanatumia Sabun

Sijafa-sijaumbika....

Si nikaumwa Tetekuwanga!!! Isije siku tunakutana ukaanza kunifokea/Suta kwanini nilisema nina ngozi nzuri wakati nimejawa na madoa ka Chui(as if unajali). So wacha nijihami mapemaa. Sikutegemea kuwa siku moja ningeugua Ugonjwa huu so nilipoanza kuumwa nkasema Mimba nini? Unajua....unapofanya Mapenzi nyama kwa nyama na Mumeo kitu cha kwanza kuangalia ni Mimba kila unapojisikia vibaya ili nisijetumia Madawa nakuua au kulemaza Kiumbe(sio kwamba naitaka hiyo Mimba). Ndio hivyo sasa nimeugua gonjwa la Kiwahili(sio kweli).....akati nakua kuna watu (Majirani zetu) walikuwa wanatukuza magonjwa ya Kudumu kama vile Moyo,Kisukari nakadhalika. Utasikia "sie hatuumwi magonjwa ya Kiswahili kama Tetekuwanga, Typhod, Kifua kikuu na mengine yote ya kuambukiza. Tunaumwa Magonjwa ya maana kama vile Kisukari, Saratani, BP" hihihihihi.....sijui ulikuwa utoto wao au ujinga wao? Sitoki nje bila kujipaka tope(foundation) kuficha Madoa Meusi usoni....naaa hakuna kujiamini hapa.....natisha hahah

Chanya....Wanaume na tofauti zao (SY2)!

Hai? Baada ya sehemu ya kwanza iliyofunikwa na Hasi (bado ninazo kibawo though)nimeona sio mbaya tukiangalia zile tofauti ambazo ni Chanya. Bila kupoteza muda twendeeee! Wanakufia kimahama mpaka hawajielewi lakini sio ki-Romeo....hawa jamaa hawajui kuweka wazi hisia zao wazi kwa kukuambia wanakupenda na kukunidi na kukumisi kila siku, na Kamwe hutowasikia wakisema "bila wewe maisha yangu ni bure". Utakuwa umeambiwa/umesoma mahali kuwa Mwanaume asipokuambia hivyo ujue hakupendi.....sio kweli! Pili, wanafurahi kuonekana kama Familia, yaani siku hizi zile "date night" sijui "outings" hazipo.....kila mkitoka basi na wanenu pembeni. Ukimkumbushia "sisi"anakuambia "watoto bado wadogo kwanini tuwe wa binafsi na kujitoa wenyewe?"(family man?). Tatu, Tangu mmefunga Ndoa hakaribishi rafiki zake ambao ni Single na ukaribu wake kwao unapungua. Sio kwamba anaogopa watakuiba bali anajihisi kuwa kwenye era nyingine ya Maisha yake. Nne, Mara ya m