Hai?
Baada ya sehemu ya kwanza iliyofunikwa na Hasi (bado ninazo kibawo though)nimeona sio mbaya tukiangalia zile tofauti ambazo ni Chanya. Bila kupoteza muda twendeeee!
Wanakufia kimahama mpaka hawajielewi lakini sio ki-Romeo....hawa jamaa hawajui kuweka wazi hisia zao wazi kwa kukuambia wanakupenda na kukunidi na kukumisi kila siku, na Kamwe hutowasikia wakisema "bila wewe maisha yangu ni bure".
Utakuwa umeambiwa/umesoma mahali kuwa Mwanaume asipokuambia hivyo ujue hakupendi.....sio kweli!
Pili, wanafurahi kuonekana kama Familia, yaani siku hizi zile "date night" sijui "outings" hazipo.....kila mkitoka basi na wanenu pembeni. Ukimkumbushia "sisi"anakuambia "watoto bado wadogo kwanini tuwe wa binafsi na kujitoa wenyewe?"(family man?).
Tatu, Tangu mmefunga Ndoa hakaribishi rafiki zake ambao ni Single na ukaribu wake kwao unapungua. Sio kwamba anaogopa watakuiba bali anajihisi kuwa kwenye era nyingine ya Maisha yake.
Nne, Mara ya mwisho kukusifia ni siku ya kwanza kukuona lakini akikununulia zawadi lazma itaendana na style yao hata kama ni kwa mbali...ameisha kupata asa akusifie ilibiweje (adhaniavyo yeye).
Tano, kinachowatoa nyumbani ni Kazi au shughuli nyingine muhimu....lakini anachofurahi ni kuwa nyumbani na familia yake.
Sita, Pamoja na kuwa hawajui kuongea au kujieleza au wapi wakusisimue bado wakipanda Kiunoni hawatoki mpaka wahakikishe umegusa Kibo n....!
Saba, wahatumii "kama hutaki kunipa basi hunipendi" au kusema "mie nitaoa baada ya miaka 5" (huyu anakuambia sina mpango na wewe na sidhani tutavuka miaka 5 pamoja).
Nane, wanaweka extra protection ili wasikutie Mimba.....sio kwamba hawakupendi au wanadhani wewe una Magonjwa/Mchafu la hasha. Hawapo tayari kuwa Baba at least not with you (si umshukuru Mungu sasa).
Tisa, Huwasikii wakisema Mama yangu hivi au vile.....wanatambua kuwa wewe huchukui nafasi ya Mama zao na wanakuheshimu na kukuchukulia wewe kama wewe bila kutoa mifano ya Mama zao wapenzi.
Kumi, Kabla hawajafanya maamuzi makubwa/madogo wanakuhusisha ili kupata maoni yako.
Ahsante kwa kuichagua Blog hii.
Babai.
Comments