Skip to main content

You know you are the oldest...

....when Viongozi wote ni umri wako au wadogo kwako,


Unakumbuka May 2, 1997 Tony Blair alikuwa Waziri Mkuu mdogo  UK? Alikuwa kundi moja kiumri na Mama yangu ila sawa na Dingi. Hapa nilipo najihisi kama mama alivyojihisi mwaka huo(well I was not her then so I don't really know how she felt).

 
Awali, binafsi nilihisi nipo nyuma ki-career kwasababu nilichukua time off kulea wanangu badala ya kuachia Childcare industry, sio hivyo tu kufanya kazi halafu mshahara wote unaishia kwa Walezi wa watoto wako ni dhambi. Yaani unabaki masikini halafu wakati huohuo huwajui wanao na wao hawakutambui kwasababu hujawahi kuwalea. Mbaya zaidi wakikua wanakuchukia na kumpenda Miss Amanda, kumsikiliza Mr Cook and  kumuheshimu Mrs Mcmun huku wewe ukishangaa na kujiuliza kwani nimekosea wapi? Kwanini tabia  haziendani na Values zenu(baba na mama). 


Mara pap! Nikakumbuka, Wakati wenzangu akina Macron, Jacinda wa NZ (alikuwa mdogo zaidi ila kazi ilimshida), Sanna Marin wa Ufini, Georgia Meloni wa Italia, Viongozi wa UK (baada ya Boris wote wadogo ila ni wa ovyo ovyo kama maCCM hawastahili heshima ya kutajwa) wanaongoza vyama na nchi, mie nipo busy na-shape vijana wa Taifa lijalo. 



Sasa wapo Secondari wananifanya nikumbuke enzi zangu, nafurahi tumefika kwenye umri tunaongea na kujadili topics kama watu wazima, hasa wakati nawafundisha. Kipindi wapo Msingi bana, ilikuwa ngumu sana kuelewana kwasababu technically kielimu nilikuwa mbele as nilisoma Masomo tofauti  zaidi ya 7 tangu nipo la 3.😪


Kabla sijakaa vizuri wanangu wakubwa wakanikumbusha  kuwa nimezaliwa Karne ya 19, wakasema "are you that old mum"? Hawa ni ndio mnawaita Generation Alpha?  
Nikawaambia, yes kids, I am 30+ years older than you lot, even though I don't look it(in my head). Enough about me, how are you doing? 


Unaogopa uzee au umejikubali na kumshukuru Mungu umefikia umri huo na kupata uzoefu wa kuwa "middle aged" maana sio kila mtu anabahati ya kufika hapo ulipo. Pia unapata nafasi ya kukumbuka enzi zako hakukua na stress za social media,  overflow of useless information, ukosefu wa ajira, Utapeli wa high wealthy life, soft life, kujiajiri, uuzaji wa Kozi/Maombi ya kuwa tajiri/kupata ajira ambazo hazipatikani, different kind of life style trends oooh bila kusahau possions za kuvutia Wanaume wenye mahela, high value men(not high quality) kutoka South Afrika na Congo and  Kozi za Women's health na Pain management kutoka America. 


Yaani Dunia imekuwa kijiji, kila mtu anamjua mwezio kiundani na matatizo yake japo wanaishi Mabara 7 tofauti. No wonder Vijana wa leo wadogo zangu wapendwa wana kongoroka haraka, Mwanamke/Mwanaume wa miaka 28 ni kama 54. Terrible.


Anyways, kuwa makini usipotee kiimani halafu baadae uanze kujitafuta na kudhani Mkeo/Mumeo na watoto wenu wamekuchelewesha kufikia Malengo yako so unawaacha ili ukaanze miasha upya somewhere. Si unajua ile  trend ya "I come 1st, gotta love myself 1st"....well is not for you who brought other innocent people in your life, Watoto.

Heri ya Mwaka mpya 2024!

Bai.

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao