Friday, 14 November 2014

Wale "naenda Africa", Natoka Africa....

Unawajua?

Huwa hawasemi Nchi zao.....mf: unauliza (kwa kizungu) unatoka wapi? Wanasema "Africa"....where about in Afrika...."East Africa"....yes...where exactly?

Sasa tangu Ebola ime-"cotton fire" Afrika inaitwa the Land of Ebola....hihihihihi watu hawasemi tena wanatoka Afrika bali Tanzania au nchi yeyote ambayo sio Magharibi ya Afrika (au karibu)!

Kuna jamaa enzi akiwahi kusema (na wakamuamini) kuwa yeye anatoka Afrika, akaulizwa Afrika wapi....akasema "a small Country inside Tanzania called Tabata" na Baba yake ni King of Tabata!


Mie siipendi Tanzania Kisiasa(sipendezwi na Siasa za Tanzania), lakini naipenda kama Nchi niliyozaliwa, na ndio maana sina (nimekataa) Ganda Jekundu kwa makusudi kabisa....(Kwa faida ya Wanangu)!Nilivyojihami hapo juu!


Babai.
Mapendo tele kwako...

Thursday, 13 November 2014

Vyombo vya Wageni....!

Vinakaa Kwenye kabati KUUUUUUUbwa sebuleni (I used to hate that thing)....ila nilikuwa naelewa kwanini wengi wao (nilikuwa mtoto so simo) huwa na Kabati la vyombo (vitumiwavyo only wageni wakija) Sebuleni.


Nyumba nyingi za kupanga ama Mna-share jiko au kila mtu anapika Sebuleni kwake kama sio nje ya mlango wake pale Koridoni/kwa nje, hivyo kuwa na Kabati la vyombo Sebuleni inaleta maana(Wapangaji sita, wote muweke makabati yenu jikoni? Hapatatosha).
Achana na hilo...turudi kwenye "vyombo vya wageni"....mpaka leo (well mwaka juzi niliponunua Gold China Dinning Set and Tea Set*) ndio nimeelewa umuhimu wake.

Kuwa sahihi naweza kusema nimejua umuhimu wa viatu vingi baada ya kuwa "Temp house wife", vitu kama vile kusafisha nyumba mara kadhaa kwa siku (nlikuwa nasafisha once a week, ile deep cleaning).

Sasa nikienda madukani, lazima nikasalimie kwa akina "Home Departments"....yaani hadi nimeanza kuwaza mambo ya kuwa "Part time Interior Designer"
Je, unataka ku-feature? Weka maelezo yako kwa kifupi ambayo ni maisha halisi na unauzoefu nayo....fundisha au kuonya in kuchekesha way.... weka kwenye email halafu bonyeza Send.Babai!
Mapendo tele kwako...

Sunday, 9 November 2014

Kuchamba or Kutokuchamba (kwa Maji)

Wewe una prefer ipi?


Kabla ya Waarabu (Wachamba kwa Maji) na Wazungu(Wachamba kwa Karatasi)....Watu walikuwa wakitumia Majani au Mchanga kujiswafi baada ya kushundi(Kutoa haja kubwa).

Tulikuwa (utotoni) tunatumia "karatasi" (toilet tissues) siku maji yakikatika. Maji na Mkono ni sehemu ya "utamaduni" (ambao tuliletewa na Waarabu) na baadhi ni Usafi.

Hii haina Uzungu bana, ila mambo ya kushika mavi yako moja kwa moja mie hata sipendezwi nayo!....angalau ukitumia "tissue" huyashiki mavi moja kwa moja pale mahala.

Baadhi ya watu hudai kuwa wasipotumia maji hujihisi "sio wasafi" huenda ni kutokana na Mazoea au....well nenda karudie kuchamba tena kwani ni wazi umeacha mabaki.

Ukitumia muda wako vizuri baada ya kushughulika utakuwa msafi(usisahau kuosha mikono kwa kutumia Sabuni hataka kama hujagusa Shundi lako).

Kwanini nakuambia hivi? Well ni kwasababu ya Wanangu...najiuliza niwafunze kutumia Maji au niendelee na Karatasi?

Lakini kutokana na Mazingira waliopo kutumia maji itakuwa trick (sitaki kushika mavi hata kama ni ya wanangu) au a bit confusing kwao kwani kwa marafiki zao hakuna "utamaduni huo", Mashuleni haipo (unless ni shule ya Kiislamu) in which hawatokwenda.
Na-sound Mzungu sana eti?!!! Hii haina uzungu ni Logic tu.....Kutumia maji wakati unashika Mavi yako direct sio Usafi hata kama utaosha Mikono baada ya hapo!

Nakuona hapo unataka kuleta habari za "mbona Qatar kuna facilities za kuchambia bila kugusa eneo la kutolea kinyesi" au "when I was in Dubai"..... ntakutukana.

Baadhi ya Hoteli pale Dar kuna facilities za kuchambia (zina-flash mavi outta your O) but how many of us live in Hotels....eti?!!


Babai.
Mapendo tele kwako...

Friday, 7 November 2014

Inapendeza sana na unapata hisia maalum za kipekee unapokutana na "High End" new publication wanazugumzia kitu ambacho wewe(Mimi) "nisiejulikana End" nimekizungumzia Mawiki na Mawiki yaliyopita!

Unakumbuka Feminisim?hiyo ilikuwa Wiki iliyopita so achana nayo!....unakumbuka "kujilinganisha/fananisha"?.....aaah Dinah naona mbali sana ujue, nafaa kuwa Rais wa KissWay?!!! (*nimeacha kuchapa nacheka kwanza*).

Pengine bila kujua unachapisha maelezo ya siku yako ilivyokuwa "njema" au unaweka picha au unaweza tu ku-share ulichonunua wiki hii kwa ajili ya wanao au mwenyewe n.k.....ni sehemu ya maisha yako hivyo unadhani ni poa tu uki-share na watu wanaofuatilia "kurasa" yako popote ulipo kwenye Social Media.

Kuna mahali unafikia unakuwa karibu sana na watu hao ambao huwajui(mnakuwa connected), sometimes mna-miss-iana.....Jinsia tofauti hapa lazma "lust" au hata "love" hujitokeza....duh! Nilikuwa nazungumzia nini kwani? Mweeee.....!!!

Oh, nimekumbuka....Baadhi ya wafuatiliaji wako (au wewe mwenyewe maana Sosho midia ni 2ways) ama wanaumia kwasababu hawawezi kuwa na maisha ka' wewe au wanataka kuwa na maisha kama wewe au wanataka kukupita au kuonyesha kuwa wamekupita.....hapo sasa Kujilinganisha/Kujifananisha kunapojitokeza.

Hii sasa inachangia kwa kiasi kikubwa kupunguza hali ya kujiamini kwa baadhi ya watu, wanakosa raha na kujiongezea msongo wa Mawazo.

Ongezeko la Kipato kwa Wanasaikotherapi na ni Tenda mpya ya Wa-Famasia kuja na Dawa ya "disorder" hii mupya iitwayo CCD(Constant Comparison Disorder"....ambayo inaharibu maisha ya watu.

Ujue Maisha ya Kawaida ya Ulayani nilipo ni Luxury kwa baadhi ya watu huko nilikotoka, sasa sio mbaya kama tukijaribu ku-limit tu-share-ayo na wenzetu hasa wale wa Kunyumba!
Hivi by the time nafikisha Miaka 50, Cosmetics surgery si itakuwa imeshuka bei?!!!Babai
Mapendo tele kwako...

Thursday, 6 November 2014

Zawadi kutoka kwa Mwenza!

Kwa siee wa Ulayani huwa tunapenda sana zawadi kutoka Nyumbani, zawadi (Radha ya Nyumbani) kama vile Ubuyu, Mahindi Mabichi*, Matembele ya Kukausha, Dagaa wa Kigoma, Viuongo vizima vya Pilau, Maembe Dodo au Embe Tanga bila kusahau Embe Ngong'a(unazijua?!!), Maharage ya Mbeya au yale ya Njano, Njugu Mawe n.k.

Mimi binafsi huwa napata hizo mavitu moja kwa moja kutoka kwa Mama, lakini kwa wale wenye Wenza wanaopenda kwenda Bongo Mara kwa Mara huwa wanavipata moja kwa moja kutoka kwa Wenza wao.

Tatizo ni kuwa Mwenza anapokuletea zawadi wakati mwingine inakuwa imetoka kwa Mme/Mke mwenzio bila wewe kujua.

Inasemekana wenzetu walioungana na "rangi" tofauti huwa wana-miss sana "rangi" yao hivyo wanaporudi Nyumbani huwa rahisi kupata wanawake/wanaume ambao huwapatia kile wanachokikosa kutoka kwa wenza wao Weupe....Maisha yaha....namaanisha Haya!!!

Halafu kuna wale ambao wanapenda tu kulala hovyo(Malaya)....Ujue! Ili uendelee kuwa interested na Kimada wa Kiume/Kike kila unapotoka Ughaibuni ni vema kuonyesha unaipenda Familia yake (ili akuamini) na hapo ndipo suala la Zawadi linapokuja!

Mke/Mume anarudi kutoka Bongo na makilos ya kila kitu nilichokitaja hapo awali, hadi dawa za Miti shamba.....hihihihihi mambo ya "radha" ya nyumbani!

Mwenyewe unapokea kwa furaha ukidhani zatoka kwa mwenza kumbe ni kwa Mke/Mume mwenza! Mara unaanza kumchukia Mumeo/Mkeo bila kujua sababu.....hehehehehe.

Kabla hujanijaji! Mama amekuwa na tabia ya kuniandalia mavitu hayo akijua naenda au kuna mtu anaenda so nina uhakika havitoki kwa "mwenza" bali Mama yangu mpendwa.
Halafu anavyojua kuvifunga sasa, hehehehe nadhani ni kwasababu ya "security" Uwanjani.....amekuwa akifanya hivyo Tangu sijakutana na Mume wangu. Enzi nasoma!Isitoshe hakuna mtu anakula "radha" ya Nyumbani bali mimi peke yangu.


THE POINT is........


Babai.
Mapendo tele kwako...