Wednesday, 5 July 2017

Rudisha Heshima Ya Ndoa: Mwenza hana Jema, kila siku Kukosoa...Kukosoana ni jambo jema na muhimu ili kusaidia kurekebisha Tabia ndogo-ndogo ambazo ni mbaya lakini kumkosoa  Mwenza wako mara kwa mara (kupitiliza) bila wewe mwenyewe kujali kuwa unakasoro zako ambazo anazivumilia ni wazi utakuwa Mnyanyasaji. Unyanyasaji huo utamfanya mwenzio kujisikia vibaya na hivyo kusababisha:-

-Maumivu ya Hisia na Akili.
-Kumfanya Mwenzio ajione hana thamani au Umuhimu kwenye Ndoa yenu.
-Uoga/Hofu  kwenye Ndoa yenu
-Kuondoa Furaha na hivyo kujitenga kihisia
-Kukosa Amani
-Msongo wa Mawazo


Kwasababu Mwenza wako sio Mlalamishi au Mkosoaji wa mara kwa mara haina maana kuwa wewe ni Mungu na hukosei, kwamba wewe ni next to perfect(hakuna binadamu asie na Kasoro) ndio maana Mkeo/Mumeo hajawahi kukukosoa au kulalamika.


Ukweli ni kuwa, baadhi ya Weza huwa "wanakurekebisha" kwa vitendo, kwamba anafanya exactly vile unapaswa kufanya au kwa kukupa "hints" bila kuumiza Hisia zako wala kusababisha ujisikie vibaya. Asipo pata matokeo ndio anaweza kukuambia.

Ni vigumu sana kuishi na Mwenza wa hivyo kutokana na maumivu anayokupa. Sasa kabla hujaanza kupanga namna ya kuikimbia Ndoa yako, tulia kwanza nikuambie nini cha kufanya, Jinsi ya kuepuka....ila kabla tuanze na sababu zinazoweza kupelekea Mwenza kukukosoa kupita Kiasi(kuku nyanyasa Kihisia/Kiakili).


Nini hasa huwa kinasababisha Mkosoaji kupitiliza?

-Hawana raha/furaha na jinsi walivyo na hivyo wanataka na wewe uwe kama wao bila kujua.

-Majuto; inawezekana kutokana na Makosa yao ya Maisha huko nyuma kabla yako.

-Fainali Uzeeni, hajafanikiwa kukamilisha Ndoto zake na hivyo anatupia "Mpira wa lawama" kwako kama sababu ya yeye kufeli/kutofanikiwa(Wakati hukuwepo wakati wa Ujana wake).

-Malezi/Makuzi  mabovu aliyopitia....ama hakulelewa na Wazazi moja kwa moja  bali Ndugu kama vile Dada/Kaka/Bibi/Babu n.k. kwa zamu,  kwamba hakuwa na "Stable family" utotoni mpaka utu Uzima.


Nini cha kufanya:-

-Usiwe Hasi kwake wala kumkosoa(rudishia). Mwache atiririke na wewe Msikilize kwa makini ili upate materials/points za kutumia Moto wake ukipoa. Usisababishe Mabishano hasa kama mna Watoto.

-Utakuwa umeumia sana kihisia(kwa kawaida kama Mwanamke utakuwa umemchunia), pamoja na maumivu hayo jitahidi kufikiria yote anayokukosoa/lalamikia kila siku. je yanajirudia? je kuna mabadiliko umefanya(jirekebisha)? je haoni jema pamoja na kuwa umejirekebisha? je alikuwa amekunywa kidogo?( ona point ifuatayo hapo chini)

-Baada ya Maumivu/Mnuno/Chunio kuisha, Mwambie ungependa mzungumze. Utakapo anza kuzungumza nae mwambie wazi kuwa ungependa mzungumze na sio mbishane, kwamba akusikilize.

-Ongea nae kwa Upole lakini kwa kumaanisha tena kwa kumuangalia Usoni moja kwa moja. Mwambie tabia yake ya kulalama/kosoa kila akipata nafasi inavyokufana ujisikie. Weka wazi kuwa huna furaha tena kwenye Ndoa yenu kutokana na Tabia yake hiyo mbaya(nafasi yako kumkosoa hii, itumie vizuri. Simamia kwenye yeye kukukosoa kupita kiasi na alivyokufanya ujisikie, mengine save ili usimuumize).

-Mwambie ni sawa kukukosoa lakini sio sahihi kurudia yaleyale kila mara bila kuangalia kama umefanya mabadiliko, pia sio vema kila mnapokuwa pamoja yeye ni kukosoa tu. Mwambie hudhani kuwa hakuna jema hata Dogo ufanyalo na kustahili kukusifia/shukuriwa. Mpe mfano wa Mema unayodhani unafanya kwenye Ndoa  yenu au kwenye Malezi ya Watoto wenu.

-Malizia kwa kusema, nisingependa Ndoa yetu iishie pabaya na nisingependa watoto wetu wawe wanakusikia ukilalamika kila siku kwa mambo yale yale au pengine kusingizia ili upate nafasi ya kukosoa.


Una nyongeza? swali je? tupia humu dinahicious@gmail.com
Sijibu Email moja kwa moja bali nitaweka hapa kwa faida ya wengine.
Nathamini na kujali Muda wako hapa, ahsante.

ooh Post ijayo itakuwa Jisni ya Kuepuka Ukosoaji wa Mara  kwa mara, Usikose
Bai

Tuesday, 4 July 2017

Sababu nyingine kwanini tunawachukia Mawifi....

....(Dada wa Wenza wetu) wa sasa au waliopita(Ex), hasa kama mlizaa kabla hamjakutana au  kabla ya kuachana. Kama uliikosa ile ya mwanzo isome hapa. Hello, ipo jambo?

Madada huwa na viherehere bin vimbelembele vya kutaka kujua kila kitu, hasa Uhusiano ukiwa bado Mpya tangu kuanza/kuisha. wanaweza kujifanya wapo karibu na wewe na wanakupa support, wanakujua na kukupoenda blablabla.


Mawifi hao hao bado ni Shangazi wa Watoto wenu na ni Kaka wa Ex/Current Mumeo,  kwa maana hiyo bado watakuwa karibu na yeyote atakae kuwa na Kaka yao. Hivyo basi kuambiwa/shuhudia mambo mengi/kupewa ripoti kuhusu Mjaza nafasi(mke/Mpenzi mpya) na watoto wake na wakati huohuo wapo karibu na wewe Ex na Watoto wako.


Sasa kama wewe ni Ex au Current one mwenye utimamu hakika utaanza kujiweka  mbali na Mawifi kwa sababu chache zifuatazo:-

-Hawachelewi kukulaumu kuwa umembadilisha Kaka yao.

-Watakuwa wanazungumza na Kaka yao kuhusu Wifi yao wa Sasa na watoto wake na kamwe hawatokuambia(kama wewe ni Ex).

-Watakuwa wanajua kila kitu kuhusu Ex wa Mumeo na watoto wao bila wewe kujua...hasa kama sio muumini wa Blended family(ikiwa wewe ni Current).

-Wanapenda kujimilikisha Watoto wako na kukutenga wewe Mama yao(kama wewe ni Ex).

-Wanaibua Drama bila sababu ya Msingi(wote).

Nini cha kufanya ili kuepuka hayo na mengine uyajuayo:

Pamoja na kuwa Kijamii  Familia Mbili huwa Moja, kwamba mnapofunga Ndoa (au kuwa kwenye Uhusiano wa  muda mrefu) haina maana kuwa hao ni kweli Ndugu zako. Hata siku Moja usijifanye wewe ni Ndugu moja na Ndugu wa Mumeo(kabla hajawa Ex), hata kama wanakupenda kama Peremende.

-Hakikisha Familia yako hajiweki karibu nao
-Waheshimu kama wanavyo kushehimu au kama Dada wa Mumeo, kumbuka Upendo haulazimishwi kama hamja-click  usijipendekeze.

-Kama ni watu wa Drama, wachukulie kama walivyo(a.k.a dharau) na punguza mawasiliano. Kumbuka Wifi hawezi kuwa rafiki hivyo usijiachie sana hata wakiomba radhi.

-Weka mipaka linapokuja suala la Malezi ya watoto wako, ikitokea wameenda  kutembea kwao, wasipofuata matakwa yako, wapige Stop kuchukua wanao(wapwa zao).

-Usiogope kusema Hapana/Sitaki.

Una swali? au Nyongeza?....shoot/share nami dinahicious@gmail.com
Nitaweka hapa kwa faida ya wengine. Ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Bai.

Monday, 3 July 2017

Rudisha Heshima ya Ndoa: Mfanye Mkeo ajihisi Malkia...


...Mengi ni yaleyale yanajirudia.....kukumbushana sio mbaya, kwavile tunatofautiana ni wazi kuwa Mkeo atakuwa  na vijimambo vyake ambavyo anapenda kufanyiwa ili kujihisi kuwa yeye ni "Malkia". Umalkia ninao uzungumzia hapa sio ule wa kuishi kwenye Jumba kubwa zuri lililojaa watumishi au kumfanya Mumeo kuwa Mtumwa kwako....la asha! Habari gani?


Kwa kawaida Wanawake(wake) huwa na tabia ya kujitahidi kuwa Wake wema, tunafanya mengi sana kwenye Ndoa(au Uhusiano) na Familia(kama mmebarikiwa Watoto) wakati mwingine kama sio mara zote huwa tunasahau kuwa nasi pia tunahitaji kujisikia kama ambavyo tunawafanya Waume zetu kujihisi Wafalme.


Soma Jinsi ya kumfanya Mumeo ajihisi Mfalme kama uliikosa.


Kama kawaida kwenye haya mambo hakuna Kanuni hivyo jaribu haya kama hujawahi na hakikisha unamsoma Mkeo vizuri ili kujua ni kitu gani hasa anahitaji kutoka kwako kama Mumewe.

-Pamoja na kuwa anapesa zake, mgawie kiasi cha Pesa  zako bila sababu.....weka mahali ambapo ataziona kwa urahisi lakini atakuwa "suprised" na andika "hizi zako, tumia utakavyo", kwa Mfano. Badili ujumbe kila mara unapofanya hivyo.


-Onyesha/toa Shukurani kwa  kazi yake ngumu ya kutoa Malezi mazuri anayowapa watoto, hasa pale unapoona Watoto wanajiamini lakini wana Nidhamu(kuna tofauti kati ya kujiamini na kuwa mtovu wa Nidhamu), kama ni Mama wa Nyumbani. Kumbuka Malezi ni jukumu lenu w ote kama Wazazi lakini kwa Kawaida Mama huchangia zaidi ya Baba, hasa kama Mama huyo ni wa nyumbani.

-Onyesha(onesha) unajali anapokaribia na anapokuwa Hedhini, jifunze namna ya kumpa support, kipindi hiki huwa kigumu kwa baadhi ya Wanawake kama ambavyo ma-teenager huwa japokuwa ni kwa muda mfupi.

-Sifia Mapishi yake na sema Ahsante kila anapokuandalia chakula.

-Usishindane au kulinganisha  "attention" anayotoa Mama kwa  Mtoto/Watoto wenu, wewe ni mtu Mzima unaweza kujihudumia. Watoto bado wanajifunza na wanahitaji "attention" zaidi yako. Mkeo sio Mama yako bali  Mpenzi wako ambae pia ni Mama wa Watoto wenu. Usisahau.

-Mpeleke Manunuzi(Madukani) kila baada ya Muda fulani....sio kwenda kununua Chakula bali mahitaji yake binafsi kama vile Vipodozi, Manukato. Pads n.k,

-Anapokuambia  jambo "serious" hata kama sio hivyo kwako. Msikilize mpaka Mwisho ndio uulize swali, usiulize maswali katikati kabla hajamaliza anachokuambia. au Jitahidi kumsimamisha kwanza alafu ndio uulize....usiulize kwa kuingilia. hii itakusaidi kumuelewa zaidi.

-Jifunze Mzunguuko wake wa Ngono ambao unaenda sambamba na wa Hedhi...zile siku ambazo anakaribia ndio muda Mzuri wa wewe "kulianzisha"....kwa muda wa siku 12 tangu Hedhi kuisha Mkeo hupoteza hali ya kutaka Tendo, sio kwamba hatamani bali anahitaji "msaada" ili kutaka Tendo hivyo ongeza ujuzi kwenye kumuandaa ili kumsaidia kufurahia Tendo atakapokuwa tayari.

-Onyesha au sema adharani kuwa yeye ndio Boss....mf; Dukani, mmenda kununua Kapeti au Gari, pamoja na kuwa Muuzaji anasisitiza ununue na unajua umelipenda lakini Mkeo anaonyesha kusita, mwambie Muuzaji "huyu ndio Boss wangu, Uamuzi wake ni wa Mwisho".

au Mmekutana na "Rafiki" yako ambae hamjakutana kwa  muda mrefu, rafiki anakuomba mkutane Pub, wewe hukupanga kwenda huko siku hiyo, unamrushia Mpira Mkeo..."Mpenzi ulisema baada ya hapa unataka kwenda wapi?".....mkeo atasema atakako hata kama hakuwa na mpango huo, atajua kuwa hutaki kwenda Pub na huyo Mtu.

-Muachie afanye maamuzi kwenye mabadiliko ya Nyumba(ndani), Mambo ya kununua Pazia, Sahani, Sufuria na Mashuka haikuhusu.

-Punguza ukaribu au poteza marafiki wote wa Kike, hata kama ni Dada zako(just saying, females are snakes, I don't even trust myself kama Wifi/Rafiki kwa Wanaume hihihihi).

-Msabahi na Muage kwa Busu na/au Kumbato.....usisahau kumpigia  Simu kumjulia hali unapokuwa mbali na Nyumbani.

-Mueleze(wasiliana) kwa uwazi kuhusu Hofu zako, Shida zako....misukosuko ya Kikazi/Biashara. Hakuna mambo ya "kiume nakabiliana nayo mwenyewe"huyo ni Mkeo ni ubavu wako, mshiriki wako, Mshauri na mtu pekee anaekujua kiundani kuliko hata Wazazi wako...anaweza kukusikiliza na pengine kukusaidia kuondokana na baadhi ya "mambo ya Kiume".

-Usimkosoe/Fokea kabla hujaua sababu ya yeye kufanya alichokifanya au kilichopelekea Mtoto kuumia ambapo wewe unadhani ni Kosa, jifunze kuwasiliana bila kumfanya Mkeo ajisikie vibaya.


Nisikuchoshe si eti?

Una swali? shoot at me on dinahicious@gmail.com. Kumbuka nitakujibu  hapa kwa faida ya wengine wenye swali kama lako na sio kwa Email. Shukurani kwa kuichagua Blog hii, tambua kuwa nathamini na kujali Muda wako hapa.


Bai.