Kuna baadhi ya watu wameumbwa/zaliwa kuwa Washindani na hivyo kwao ni kawaida(pia ni vizuri), mara nyingi huliweka hili wazi mwanzoni kabisa mwa Uhusiano. Wakati mwingine wewe mwenyewe unaweza tu kugundua kuwa Mpenzi wako ni Mshindani kwenye shughuli zake za Kibiashara/Kazi, Masomo, Utunzaji wa Pesa, namna anakutunza n.k. Lakini hutofikiria hata siku moja kuwa mkifunga Ndoa hatokubali wewe "umshinde" kwenye jambo lolote. Ukiachilia mbali mtu kuzaliwa hivyo(mshindani) pia Ushindani unaweza kusababishwa na Mazingira, Uzoefu au Malezi. Kwa wale ambao wamezaliwa wachache au wengi (Mtoto wa Pili, Mtoto wa 3 au 5 kati ya watoto 8-10) au yule wa Pili kutoka Mwisho kati ya watoto zaidi ya 5(hii ni Uzoefu wangu binafsi mie sio Mtaalam). Pengine unaweza usigundue mpaka mtakapokuwa na Watoto, ambao huibia mambo mengi sana kati ya Wewe na Mwenza wako. Kumbuka Watoto huwarudisha nyote wawili kule mlikotokea(utotoni) na hivyo kutaka kulea wanao kama ulivyolelewa wewe