Skip to main content

Posts

Macho yane...

Jana si nilikuambia "nalikizoka" sehemu- sehemu ya Ulaya?....nkaenda kwenye Shopping Centre yao kubwa na wanangu wawili! (Siku zote huwa napita kwa nje tu). Simlituambia wa Ulaya hatuwezi "kulikizoka" Tanzania, sababu tukija huko sio Likizo tena bali tumerudi nyumbani, ni ukweli kabisa (sijui hili limekujaje hapa, tuliache)! Basi humo ndani (shopping centre) Macho yangu yamesifiwa na watu kibawoooo....hee! Mwanamke nikashanga....(Najua nina tumajicho tuzuri ila sio kiviiiiile)! Mkaka mmoja akashindwa kujizua akaniuliza "where are you from"? Nkamwambia "England" hihihihiihi nkaona NOMA! nkasema Tanzania, East Afrika, I have 2 kids and a husband....akasema "are all grown women look like you?....Fit, Nice skin and beautiful eyes?" Nkasema Yes! (Nimeitangaza Tanzania hapo) England hawayaonagi Macho yangu au dharau tu washenzi kabisa wale, mmmh! Ila inawezekana ni u-busy wa Maisha. Watu hawana habari, akili yote ina-focus kwenye £ ili ku...

Siri...

Unawajua wale akina "nilificha/nilifanya SIRI kwasababu nilikuwa nalinda hisia zako"....."Kwasababu sikutaka kukuumiza" mifano ya watu the shenzi kind of people? Halafu sasa umejua! maumivu ni zaidi kuliko ungejua siku aliyoifanya hiyo siri....well in my case, reaction yangu ni ileile ufiche siri kwa miaka 10 au uniambie masaa machache yaliyopita....AM GONE!! Siri uliyofichwa kwa Miezi/Miaka huuma zaidi kuliko kuambiwa moja kwa moja! The thing is kuendelea kuishi na mtu huyo ni sawa na kuishi maisha ya "Uongo". Usikute hapa nafichwa mambo kibao alafu kimbelembele na-blog hihihihihi, siku nikijua hata kama nimefikisha miaka 50, sisamehi aisee...hii ni karne ya 21 sio Enzi za Yesu!! Aah. Kuna mambo ya kifamilia hupaswi kumueleza mwenza wako unless unajua kabisa yatamu-affect yeye na watoto. Vinginevyo yaache huko huko "familiani". Sasa hizo sio Siri ninazozungumzia hapa, maana hazikuhusu! Si...

Karibu, jisikie upo Nyumbani....

Utawekewa "Maeneji" mabaya nyumbani kwako na maukarimu yako yaliyopitiliza yasioyojua mipaka, shauri yako! Unawajua wale wageni wanakuja kwako alafu wanaaza Ziara rasmi ya Chumba hadi Chumba, Droo hadi Droo, wanajipulizia Manukato yako na kujaribishia Viatu na Nguo zako.....WANANIUDHI sana. Wazungu wao huona sifa au sijui ni Kacha yao! Hata sielewi, kama ni mara ya kwanza kufika kwake atakupa Ziara ya nyumba yote mpaka Stoo kwa hiari yao....(Tuwaache). Ujue hapa Duniani bana kila mtu anamikosi yake, shida, raha na tabu zake. Hujui kapita wapi kutegemeana na "Imani" yake ili kujaribu kuiondoa Mikosi (kila mtu na siri yake bana). Siku unamkabidhi Nyumba yako unaanza kuona mambo hayawi mambo. ....usikute "eneji" yangu nzuri kwangu mimi na familia yangu, sasa ukinikabidhi nyumba yako nijisikie ka' kwangu alafu "eneji" yako mbaya ikai-triger "eneji" yangu nzuri na kuzalisha "sumu" yakawa mambo sio mambo usilalamike....Mfano tu...

Uelewa na kumbukumbu ya Mtoto.

Nilipotobolewa Masikio nilikuwa na Miezi Sita (kwa Mujibu wa Mama), alienitoboa ni Mama wa Kimasai na aliekuwa kanibeba/shika ni Bibi yake Mama. Sikumbuki maumivu, lakini nakumbuka nililia sana nilipomuona Mama wa Kimasai na Shanga zake na Masikio yakiwa marefu "kwenda chini". Siku niliyomsimulia Mama kuhusu hiyo siku ya tukio (nilikuwa teen na bado naikumbuka)...alinishangaa na kusema kuwa lazima nilisikia akisimulia watu, mtoto wa miezi Sita hawezi kukumbuka. Nilipokuwa na miaka 3 au zaidi, tulikuwa Mjini Mbeya....Mama, Mimi, Mjomba na watu wengine tulikuwa tunapita pembezoni mwa Mto. Mjomba wangu alinibeba na kutishia kunirusha kwenye Maji(Mto)....Nadhani ndio maana naogopa Maji....Safari zangu ni za Anga, Reli na Barabara, mie Meli sijui Boti sipandi....Mtumbwi? Bora uniue. The point is, Mtoto anauwezo wa kutunza kumbukumbu kuanzia umri mdogo sana kuliko tunavyoaminishwa na "Mzungu" the Shenzi. Sio unafanya mambo u...