Unawajua wale wageni wanakuja kwako alafu wanaaza Ziara rasmi ya Chumba hadi Chumba, Droo hadi Droo, wanajipulizia Manukato yako na kujaribishia Viatu na Nguo zako.....WANANIUDHI sana.
Wazungu wao huona sifa au sijui ni Kacha yao! Hata sielewi, kama ni mara ya kwanza kufika kwake atakupa Ziara ya nyumba yote mpaka Stoo kwa hiari yao....(Tuwaache).
Ujue hapa Duniani bana kila mtu anamikosi yake, shida, raha na tabu zake. Hujui kapita wapi kutegemeana na "Imani" yake ili kujaribu kuiondoa Mikosi (kila mtu na siri yake bana). Siku unamkabidhi Nyumba yako unaanza kuona mambo hayawi mambo.
....usikute "eneji" yangu nzuri kwangu mimi na familia yangu, sasa ukinikabidhi nyumba yako nijisikie ka' kwangu alafu "eneji" yako mbaya ikai-triger "eneji" yangu nzuri na kuzalisha "sumu" yakawa mambo sio mambo usilalamike....Mfano tu usinijaji bana eeh!
Mie bana kwangu ni kwangu, ukija wewe ni Mgeni tu....nitapika, nitaandaa kila kitu hata kama nimetoka Kujifungua jana! Nitaitafuta tu hiyo nguvu....sikupi nafasi hata!....kwa Dinah hakuna "jisikie upo nyumbani BS" kuna "karibu sana" tu.
Ukitaka kitu niulize/niombe nitakuelekeza ukachukue au nitaenda kukuletea. Kitandani kwangu huweki matako yako(hukai) utaanzia wapi kwanza, Chumbani tu hauingii(ni marufuku)!
Hata nikienda kutembelea watu huwa "sijiachii" nyumbani kwa watu na kutembelea chumba hadi chumba(Uzungu wenu huko huko), hata kama nimekaribishwa kwa "jisikie upo nyumbani".
Stori time: Mie nilisoma Kutwa sio! Sijawahi ku-share chumba wala kitanda na mtu baki (zaidi ya wadogo zangu). Nilipokuja huku nikawa na-share nyumba sio Chumba wala kitanda, so wanafunzi wenzangu wa karibu (nyie mnaita marafiki) wakija kunitembelea walikuwa wakiishia Sebuleni.
Summer moja hivi Rafiki yangu akawa amepata replacement mahali karibu na kwangu, akaomba kuja kulala kwangu ili kesho yake awahi Kazini siku ya kwanza.
Nikamwambia hakunaga noma, wee njoo tu, nikamuandalia alale Sebuleni...heee! Mwanamke wa Kighana nusura alie kisa eti nimegoma asiingie Chumbani kwangu ku-"have a look".
Ikabidi nimfunde.....Kitanda ulaliacho na Mumeo hakipaswi kuonwa au kukaliwa na mtu ambae hamjachangia Damu (isipokuwa Mumeo).....ndio akanielewa.
Last Xmas alitualika kwake...mara nikahitaji kumbadili "Mini me" Nepi! Akanipeleka Chumbani kwake....kabla sijaingia nkamuuliza, "Sandy-O is this your bedroom?" Akasema "Yes-O, make yourself comfortable, feel at home-O". Nkagoma kuingia!(silly woman).
Ukarimu ni muhimu sana Maishani lakini kama ilivyo kwenye kila kitu, tambua mipaka au jiwekee "Mipaka" ya Ukarimu wako.
Babai.
Mapendo tele kwako...
Comments