Thursday, 3 July 2014

Macho yane...

Jana si nilikuambia "nalikizoka" sehemu- sehemu ya Ulaya?....nkaenda kwenye Shopping Centre yao kubwa na wanangu wawili! (Siku zote huwa napita kwa nje tu).


Simlituambia wa Ulaya hatuwezi "kulikizoka" Tanzania, sababu tukija huko sio Likizo tena bali tumerudi nyumbani, ni ukweli kabisa (sijui hili limekujaje hapa, tuliache)!

Basi humo ndani (shopping centre) Macho yangu yamesifiwa na watu kibawoooo....hee! Mwanamke nikashanga....(Najua nina tumajicho tuzuri ila sio kiviiiiile)!

Mkaka mmoja akashindwa kujizua akaniuliza "where are you from"? Nkamwambia "England" hihihihiihi nkaona NOMA! nkasema Tanzania, East Afrika, I have 2 kids and a husband....akasema "are all grown women look like you?....Fit, Nice skin and beautiful eyes?" Nkasema Yes! (Nimeitangaza Tanzania hapo)


England hawayaonagi Macho yangu au dharau tu washenzi kabisa wale, mmmh! Ila inawezekana ni u-busy wa Maisha. Watu hawana habari, akili yote ina-focus kwenye £ ili kulipa bills, mambo ya kuishi ili kufanya kazi ulipe Bills na sio kufanya kazi ili Uishi kwa raha.


Usipanic ukaanza ku-google picha ili uthibitishe "uzuri" wa macho yangu! Uzuri wake sio ule utakao wewe......sasa relax!


Nkaingia mahali wana "pumper" na kuuza bidhaa kwa Wanawake....mambo ya Skin Scrubs, sijui Manicure kits, Hair Masks nakadhalika.....muhimu ni "all natural".

Nkapewa Kichupa (kidogo tu hivi) cha Mchanga wa Baharini uliochanganywa na Asali na Mafuta ya Nazi, kinauzwa £49.99 (karibu Laki ya Tz)....eti nkaambiwa "if you are in relationship, things will improve! Your skin will be soooo soft".


Nkamuangalia huku najisemea kimoyomoyo...."niibie kwa mengine lakini sio relationship"....nkakarudisha kachupa kake ka' Skin Scrab kwa peed ya ajabu.


Stori time: Kule kwetu Uzaramuni (not my real Kabila)....kila J'pili watu tulikuwa tunaenda kuoga Baharini "kuondoa Mikosi" hihihihi sio bana, tulienda kujisafisha Ngozi kwa kujisungua na Mchanga wa Bahari kisha kujipaka Mafuta ya Nazi.

Kipindi hicho nilikuwa bado Kabinti na aliekuwa akitupeleka huko ni Marehemu Baba.....sio nyie wa leo mnaenda kutembea pembezoni mwa Bahari mnajifanya eti mnaondoa Mawazo! Una mawazo? Katembelee Makaburi au Kanisa upate Amani.(Hili limetoka wapi kwani?)


Anyway...Mchanga unaondoa Mabaki ya ngozi iliyokufa na Chumvi inaponya matatizo Mengine ya ngozi, wakati Mafuta ya Nazi yanalainisha Ngozi. Sasa ukitaka Uterezi "feeling" na Mchanga ukung'ang'anie ili "utakate" vizuri ndio waongezea Asali.


Alafu mnaaminishwa kuwa kila kitu kizuri kwa Ngozi au Afya kimeletwa/anzishwa na Mzungu na Mnakubali!!*The husband and 2 kids bit nimetania hoping utacheka....ror!!


Babai.
Mapendo tele kwako...

No comments: