Skip to main content

Siri...

Unawajua wale akina "nilificha/nilifanya SIRI kwasababu nilikuwa nalinda hisia zako"....."Kwasababu sikutaka kukuumiza" mifano ya watu the shenzi kind of people?





Halafu sasa umejua! maumivu ni zaidi kuliko ungejua siku aliyoifanya hiyo siri....well in my case, reaction yangu ni ileile ufiche siri kwa miaka 10 au uniambie masaa machache yaliyopita....AM GONE!!





Siri uliyofichwa kwa Miezi/Miaka huuma zaidi kuliko kuambiwa moja kwa moja! The thing is kuendelea kuishi na mtu huyo ni sawa na kuishi maisha ya "Uongo".





Usikute hapa nafichwa mambo kibao alafu kimbelembele na-blog hihihihihi, siku nikijua hata kama nimefikisha miaka 50, sisamehi aisee...hii ni karne ya 21 sio Enzi za Yesu!! Aah.





Kuna mambo ya kifamilia hupaswi kumueleza mwenza wako unless unajua kabisa yatamu-affect yeye na watoto. Vinginevyo yaache huko huko "familiani". Sasa hizo sio Siri ninazozungumzia hapa, maana hazikuhusu!





Siri ninazozilenga hapa ni zile zinazokuhusu kwa kugusa hisia na maisha yako mf, matumizi ya pesa, mawasiliano yake na Ex (kama kuna mtoto/watoto kabla yako), uhusiano wake na mtu ambae anajua hupatani nae (couple support each other, kama simpendi Jonathan lazima umpotezee pia) n.k.





Naamini Binadaam wote tuna Sixth sense kuna wakati unajua kabisa kuwa kuna jambo linaendelea na unafichwa, lakini unadharau.





Kudharau kwako kunamfanya "mficha siri" adhanie kuwa hujui kitu....kumbe wewe unajua kila kitu, unamlia timing tu akuambie kwa hiyari yake ili ukamilishe "Visa" ya safari.





Kale kahisia unakokapata alafu Moyo unadunda kwa mshtuko then hatua (haudundi kawaida) kale! ni sehemu ya "sixth sense"....6th sense hukujia tofauti inategemea na tukio linalotokea wakati huo au lijalo. Uisiidharau, isikilize kwa makini sana.




Nipo sehemu sehemu Ulaya "nalikizoka", nikaona maduka 3 ya Sally....Sally's brand ya Marekani....is it same as Wilknsons??!! Hata sijui....hee! Nikadhani nipo Marekani bana England hakunaga Sally"s.


Babai
Mapendo tele kwako...

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao