Ulitegemea nitaorodhesha matukio yote ya mwaka huu? Hehehehe pole. Napenda kuwa tofauti.
Ahsante kwa kuichagua Blog hii siku ya leo ambayo ni ya Mwisho kabisa mwaka huu wa 2014, Ubarikiwe sana.
Wiki mbili zilizopita zilikuwa hectic kweli, si unajua Christmas inavyokuwa ukiwa na Watoto? Hasa mmoja ambae sasa yupo "Shule" na huko anafundishwa zaidi kuhusu "Santa na Presents" kuliko Kuzaliwa kwa Yesu...Achana na hili.
Sasa tangu nimekuwa Mama nimejikuta nasoma sana Forums zenye reviews mbalimbali kutoka kwa "real people" from Vipodozi to Kampuni za Umeme.
Nikawa kwenye Forum moja ya masuala ya Wazazi, Malezi, Mimba n.k. Nikawa nasoma review za aina ya Dawa ya Kuzuia Mimba (Uzazi wa Mpango)....mwanamke sijawahi kugusa hayo mavitu.
Kama kawaida hukosi maswali ya mabinti wadongo ambao wanataka kutumia Madawa hayo, nikisema wdogo kwa huku ninamaanisha 16 kushuka chini(inatisha, najua)!
Binti mmoja akas...