Ndio na Hapana.....hello, jambo kabisa? Wengi sio wajuaji (wanajua sana)ila nadhani ni wazuri kwenye kufananisha..... ukifananisha system ya UK na Tza kwa mfano hakika uta-sound mjuaji(kumbe ni bongolala tu). Kingine kinachofanya udhani kuwa wa Ughaibuni wanajifanya wajuaji ni uhuru wa kusema, kwamba kila mtu ana Maoni yake kuhusu kila kitu kinachotokea au anachokisoma na pengine kushuhudia. Uhuru huo (ahsante nyingi kwa Gugo) unafanya baadhi yetu kuweka maoni yetu kwenye issue yeyote ambayo tunahisi inatugusa. Nikianza kukupa (maoni yangu) mbinu za kukusanya Kodi (nita-base zaidi na system ya UK ambayo naijua lakini wewe huijui) na kuitumia Kodi hiyo kwenye kuboresha Maisha ya Watanzania waishio maisha Duni hakika utaniona nina Akili kweli na ninafaa kuwa Waziri. Kumbe katika hali halisi mie ni m-bovu wa Hisabati na Masuala ya Kiuchumi siyajui lakini ni mzuri kwenye kujieleza so nikipata "material" naweza kuyaelezea kwa urahisi na kueleweka bila kutumia "stat...