Mtoto wa kambo sehemu ya kwanza.... Kambo maana yake nini? Ikiwa mtoto alizaliwa nje au kabla ya ndoa nae anaitwa mtoto wa kambo? au ni kwa wale waliozaliwa ndoani halafu ndoa ikafeli au mzazi mmoja kafariki halafu baba/mama kaoa/olewa tena? Mnaona mlivyo haribu/changanya mambo baada ya kuua umuhimu wa ndoa na kujenga familia? Mtoto kabla na nje ya ndoa (Wanaharamu) huwa hawajulikani/hawana umuhimu(kwa Waislamu hii bado imesimama). Nimekukwaza? ndio ukubwa huo.😁 Mama/baba wa kambo inatumika zaidi Mikoani, huku kwetu Pwani tunatumia sana Mtoto wa kufikia(kwamba umefika kimapenzi kwa mwanamke/mwanaume ukamkuta mtoto kutoka ndoa iliyopita?)…sina uhakia. Nitatumia maneno mtoto na watoto interchangeably. Nani alipitisha sheria ya kulazimisha watu wawapende watoto waliowakuta kwa watu waliowadondokea kimapenzi? Yaani ukionyesha huna habari na uzao wa mwanamke/mwanaume kabla yako basi unaitwa Mwanga, unaroho mbaya n.k. Utapendaje mtu wala humjui na hana faida kwako?...