Skip to main content

Posts

Mtoto wa kambo(part 1)...

Mtoto wa kambo sehemu ya kwanza.... Kambo maana yake nini? Ikiwa mtoto alizaliwa nje au kabla ya ndoa nae anaitwa mtoto wa kambo? au ni kwa wale waliozaliwa ndoani halafu  ndoa ikafeli au mzazi mmoja kafariki halafu  baba/mama kaoa/olewa tena?  Mnaona mlivyo haribu/changanya mambo baada ya kuua umuhimu wa ndoa na kujenga familia? Mtoto kabla na nje ya ndoa (Wanaharamu) huwa hawajulikani/hawana umuhimu(kwa Waislamu hii bado imesimama). Nimekukwaza? ndio ukubwa huo.😁 Mama/baba wa kambo inatumika zaidi Mikoani, huku kwetu Pwani tunatumia sana Mtoto wa kufikia(kwamba umefika   kimapenzi kwa mwanamke/mwanaume ukamkuta mtoto kutoka ndoa iliyopita?)…sina uhakia. Nitatumia maneno mtoto na watoto interchangeably. Nani alipitisha sheria ya kulazimisha watu wawapende watoto waliowakuta kwa watu waliowadondokea kimapenzi? Yaani ukionyesha huna habari na uzao wa mwanamke/mwanaume kabla yako basi unaitwa Mwanga, unaroho mbaya n.k. Utapendaje mtu wala humjui na hana faida kwako?...

Jinsi ya kujenga/kuza“character” ya mtoto wako.

Jambo wewe, Kulea Watoto Ughaibuni ambako kuna Kacha tofauti na Kacha tuliokulia nazo inaweza kuwa a bit confused, hasa kama umetoka zako Afrika (bongo as in Tz ikiwepo) na Kacha ya U-marekani mweusi. Unazaa Watoto na hujui uwalee katika kacha gani, nap engine unajiuliza hivi huku ulipo wanao wana kacha yeyote au wafuate kacha ya watu wanaofanana nao(Weusi wenzao aka Black Culture)? Unasahau kuwa kila mweusi wa Ulaya ana kacha yake aliokuzwa nao kulingana kabila lake na wapi anatokea Afrika.     Kwa kifupi nchi kama UK hakuna Black culture (wanalazimisha kuuingiza U-black Amarekan) bali kuna Culture za Afrika na Caribbean ila kwa wale wazazi waliokuja na U-black amerika kutoka Afrika basi huamini kuwa Culture ya Black amerika ndio Black culture Dunia nzima na hivyo kuindeleza. Hizo kacha   zetu za Afrika na Caribbean hazidumishwi na Taifa zaima la UK isipokuwa jamii husika ni kama ambavyo jamii nyingine ya wazungu kutodumisha Kacha zao Kitaifa kwasababu UK ina mataifa...

Huge Microphones na yupo youtube...Kero zangu.

...ndio mnaita podcasts?  wameharibu youtube eti, au nimezeeka niachane nayo kama nilivyoiacha twita? Anyways, hujambo? Unaendeleaje na u-pre-menopause? Kama binadamu hakika kuna vitu vinakukera, binafsi nakwerwa na sehemu kubwa ya jamii ya online, hasa mamilionea na wamarekani weusi wanaoijua Afrika na kacha zake zote (nchi 57?) baada ya kwenda Ghana kwa wiki moja wa youtube na mi-microphone yao makubwa ka' wapo Mawingu FM. Halafu usinikumbushe wale wanajipanga kwenye vibox(zoom meetings) wanaanza kubishana oh my days.,,,ukute ni wivu wangu tu, maana  wanangu wakienda shule na Baba yako Kazini nabaki hapa sina hili wala lile. Ukiachana na hao kuna wale young single men and women wanashauri/fundisha wenzao namna ya kuishi maisha ya ndoa(Well I did that when I was younger but kama unakumbuka nilishauri kuhusu mahusino na ngono nilikuwa in one na was doing it). Najua unatambua kua sio tu Ndoa ni tofauti na maisha ya ndoa, pia Ndoa sio mahusiano japokuwa mahusiano ni sehemu ya nd...

Kutoa ushauri wa Mapenzi, Ngono na Ndoa...Elimu, Uzoefu na Mazingira vinatosha?

  Za leo? Muibuko wa Podcast za wakaka na dada wajuzi wa maisha ya Ndoa zimekuwa nyingi na karibu wote (kutokana na uchunguzi nilioufanya) hawajawahi kuishi Maisha ya ndoa, lakini wanashauri wenzao(hasa wanawake) namna ya kuishi na Mume. Bila kutilia maanani kywa kuna tofauti kubwa sana kati ya kuishi na mpenzi na kuishi na mke/Mume.   Binafsi sidhani kuwa unahitaji Elimu….kwasababu matatizo hayo hayafanani   kwa ukaribu na hakuna dalili zinazofanana kama vile Magonjwa, matatizo ya kimaisha, afya ya akili. Mapenzi na ndoa yameegemea zaidi kwenye aina ya wahusika(muonekano/kipato), malezi, mazingira na jinsi   mhusika alivyo umbwa/zaliwa(japokuwa tunazaliwa na ubongo mtupu)…tuegemee kwenye Malezi na mazingira, maana suala la kipato na muonekano ni la majaaliwa. Pamoja na kusema hivyo Elimu kuhusu Tabia za binadamu na jinsi ubongo unavyofanya kazi inaweza ikasaidia Zaidi, ila kumbuka Ubongo ni complex na “chemical” zake zinaweza kutofautiana   kutoka kwa mtu n...