Skip to main content

Posts

Celebs

Hii jamii ina power ya ku-normalize kila kitu, hata vile ambavyo ni normal lakini jamii nyingine hawavifanyi, wao hu-normalize. Mfano ni "attachment parenting" ambapo mama analala na mtoto wake na kumnyonyesha for as long as possible. Hiyo "attachment parenting" si ni kitu cha kawaida kwenye jamii ya Kitanzania(na Afrika kwa ujulma)....nimezaa mwanangu wa kwanza nikapigwa marufuku kulala nae ili kuepusha cot death. Nikakumbuka Mama alipozaa wadogo zangu 3 wa mwisho, wote alikuwa analala nao kitanda kimoja na hakuna aliepoteza maisha.... Aii....nikawa na lala na mwanangu ka' ifuatavyo na amenyonya mpaka mwaka na miezi 3. Siku hizi analala chumbani kwake lakini akiota ndoto mbaya anakimbilia kwetu so tunalala wote wanne. Huyu wa pili bado analala na sisi na bado ananyonya (mwaka na miezi 3) tena huyu ni king'ang'anizi kuliko kaka yake ambae hakujali kulala peke yake au kulala na sisi.. Kingine ni Kuzaa kwa kupasu

Uswahili Mzigo...

Halo, haloooo....Halo ya Mbuzi meeeeee! Kuna tofauti kati ya Uswahili way of life which ni kitu cha kujivunia, ni kama "culture"....alafu kuna Uswahili "ile hali ya kutokuwa Mstaarabu" na Uswahili simply kwavile wewe ni mwafrika(Muafirika). Wenzetu wa Kishua hawapendi Uswahili kabisa yaani! Wao wanaishi Kizungu zaidi....usiniulize kwanini wengi wao wakifika Uzunguni (Ulaya, Marekani, Down Under etc) wanakuwa Waswahili kupita wale Waswahili wa Mtaani kwetu pale KissWay(Kisarawe). "Unaedha" dhani kuwa wamebadilika, hapana hawajabadilika bali kuishi "Kizungu" Ulaya inabidi uwe Posh....U-posh waenda sambamba na Pochi(mahela).....sasa inawezekana kabisa tuhela twako + rangi yako, Elimu na ulikotoka inakuwa ngumu kidogo kuishi "kizungu" kwa Wazungu.....sijui umenielewa?!!! Sasa unaishia kuishi na Waswahili wenzako "wa Kizungu" ambao awali hukujua tofauti yao kati ya Middle class, Working class, Chav n.k Kama tunavyojitenga Tanzania

Baba zetu nao...

Wiki Mpya oyee! Nimeacha kujivunia Tanzania kama Taifa(Kisiasa) miaka kadhaa iliyopita, najivunia Tanzania kama Nchi na baadhi ya Tamaduni zake, kama vile kuvaa Vibwaya (vile vifupi, kuachia tumbo na kufunika Matiti), Ngoma na nyingine nzuri nzuri. Kuna unataratibu wa baadhi ya wanaume kudai kuwa mwanamke yeyote atakaelala nae ni Mama yako na mtoto yeyote atakaezaliwa na mwanamke ambae sio Mama yako ni Ndugu yako. Sina uhakika kama ni Utamaduni,Tabia au pure______! Mama yako ni yule aliekuzaa au "kisasa" aliekulea tangu ukiwa na umri wa masaa au siku chache.....sio random women aliolala nao Baba yako. Pia ndugu yako ni yule mliotoka tumbo Moja, wengine ni Jamaa (tena ukiamua kuendeleza ujamaa huo kwani sio lazima). Tabia ya Baba kulazimisha watoto wao kuwaita wanawake wengine Mama au watoto waliozaliwa huko (kabla au baada ya Ndoa) wadogo/kubwa zao sio haki na sio sahihi kwa mtoto/watoto husika. Huyo ni Mkeo na hao ni watoto wako w

Mkorogo...

Habari... Mkorogo ni kutumia bidhaa "illegal" au "home made skin lightening" na "kujiton" ni kutumia bidhaa zilizothibitishwa na Jamaa wa Ubora wa Viwango eti?.....wote nia yao Moja. Waafrika kwa Waafrika kwa ubaguzi wa rangi zetu hatujambo....tofauti ya Ubaguzi wetu sisi Watanzania ni kuwa hatutengani au kuuana kwa sababu baadhi yetu ni weusi sana au weupe sana. Well, isipokuwa kama wewe ni Mweusi tii alafu huna nywele laini na unaishi Somalia au Sudani Kaskazini.....oh au Chotara ndani ya South Africa. Ila Machotara ndio huwa wabaguzi zaidi kwa Weusi kuliko sisi wenyewe kwa wenyewe....Usiombe ukutane na Chotara wa Kizungu aliekubaliwa kwenye jamii ya Kizungu ayeee!! Anyway, nukta hapa ni kuwa tofauti ya weusi wetu wa ngozi ndio hutufanya tuwatanie wenzetu na kuwaita majina....Mf: Cheusi dawa, Mpingo,Cha usiku n.k Huu utani huwafanya baadhi(hasa wanawake) wajisikie wanyonge, hawavutii....inafikia mahali wa